Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Philip Mangula
akizungumza na Wenyeviti wapya wa Mashina ya CCM waliochaguliwa katika
uchaguzi ndani ya Chama, uliofanyika hivi karibuni, alipokutana nao leo
katika Ukumbi wa Vijana Sodial Hall, Kinondoni, jijini Dar es
Salaam. Picha:Bashir Nkoromo.
——————
Na Bashir Nkoromo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara Philip Mangula,
amesema wapinzani hawakuwa na uwezo wa kushinda katika baadhi ya majimbo
na kata jijini Dar es Salaam, katika uchaguzi mkuu uliopita isipokuwa
walisaidiwa na wasaliti ndani ya chama.
Amesema, kutokana na madhara hayo, CCM itaendelea kuwasaka na
kuwang’oa wasaliti hao, wakiwemo wale waliofanikiwa kujipenyeza na
kushinda nafasi mbalimbali katika uchaguzi ndani ya Chama CCM na ndiyo
maana CCM imefuta uchaguzi kwenye baadhi ya kata.
Mangula amesema hayo leo katika kikao chake na Wenyeviti wapya wa
Mashina ya CCM, kutoka kata za Kawe na Kinondoni, waliochaguliwa hivi
karibuni, kilichofanyika leo Vijana Social Hall, Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Amesema, tayari chama kimeshachukua hatua mbalimbali kwa wasaliti
kuanzia ngazi ya taifa, mikoa na kata kwa kuwapa adhabu zikiwemo za
kuwafuta uanachama, onyo kali na wengine kuendelea kuchunguzwa.
“japokuwa tumekwishachukua hatua mbalimbali dhidi ya wasaliti lakini
bado kazi hii inaendelea hadi tuhakikishe tabia hii chafu ya usaliti
inakoma ndani ya chama, kwa sababu ni jambo la kushangaza CCM yenye
wanachama wengi kiasi hiki kuliko chama chochote inapoteza majimbo
katika mazingira yasiyo na majibu”, alisema Mangula.
Akitoa tathimini kuhusiana na wasaliti ngazi ya mkoa, alisema jumla
ya viongozi 4595 walikuwa wasaliti ndani ya Chama walipewa onyo, huku
3907 wapo chini ya uangalizi wa miezi 12.
Wengine waliopewa kalipio ya miezi 18 walikuwa 4, wengine 398 wapo
katika uchunguzi, 465 wameadhibiwa, huku waliofukuzwa na kuvuliwa
uwanachama wapo 2267.
Mangula aliwataka Wenyeviti hao wapya kuwa mstari wa mbele
kuhakikisha CCM inaimarika katika maeneo yao kwa kuzingatia misingi na
kanuni ambayo mojawapo ni kuepuka kupokea na kutoa rushwa hasa nyakati
za uchaguzi.
Akimkaribisha mangula kuzungumza na wenyeviti hao, katibu wa CCM mkoa
wa Dar es Salaam Saad Kusilawe aliwataka watendaji katika matawi yenye
miradi kuisimamia kwa makini midari hiyo hasa upande wa mapato, ili
mapato yanayopatikana yatumike pia kuwalipa japo kidogo wenyeviti wa
mashina.
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara
Philip Mangula akiwasili katika ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni
Dar es Salaam, kuzungumza na Wenyeviti wa Mashina kutoka Kata za Kawe na
Kinondoni, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad
Kusilawe.
Wenyeviti wa CCM wa matawi wakimshangilia Mangula alipoingia ukumbini
Mangula akiwa meza kuu baada ya kuwasili ukumbini
Wenyeviti hao wakishangilia ukumbini
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es
Salaam Saad Kusilawe akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip
Mangula, kuzungumza na wenyeviti hao wa mashina
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara
Philip Mangula akizungumza na Wenyeviti hao wa mashina kutoka katika
Kata za Kawe na Kinondoni, Dar es Salaam, leo
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara Philip Mangula akikabidhi vitendea kazi kwa
mwenyekiti wa shina namba 12 Oysterbay, James Nyakyoka, alipokabidhi
vifaa hivyo kwa wenyeviti hao baada ya kuzungumza nao jana. (PICHA BASHIR NKOROMO)
Wednesday, September 6, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakiwa wamejipanga tayari kwa maandamano katika maadhimisho ya S...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment