METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, November 10, 2019

JAFO AAGIZA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI S/MITAA KUPOKEA RATIBA ZA KAMPENI

Na.Alex Sonna,Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI Seleman Jafo amewaagiza wasimamizi wa uchaguzi kuanza kupokea ratiba za kampeni kutoka katika vyama vya siasa nchini kuanzia leo hadi kesho jioni .

Aidha,amesema tarehe ya matukio na shughuli zingine zote zinazohusu uchaguzi huo zitaendelea kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi serikali za mitaa wa mwaka 2019
Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utoaji wa taarifa ya wa taarifa ya wagombea waliorejesha fomu ,uchukuaji fomu,uteuzi,pingamizi na rufaa lililoanza tarehe 29/10/2019 hadi tarehe 9/11/2019.

Jafo amesema jumla ya waliorejesha fomu ni jumla ya wananchi 539,993 sawa na asailimia 97.3 kati ya  wananchi 556,036  wote waliochukua fomu.

Aidha ametaja orodha ya vyama vilivyochukua na kurejesha fomu ambapo wagombea kutoka CCM walikuwa 412,872 sawa na asilimia 74,CHADEMA walikuwa 105,937 sawa na asilimia 19,CUF walikuwa 24,592 sawa na asilimia 4,ACT-Wazalendo walikuwa 8,526 sawa na asilimia 1.5,NCCR-Mageuzi walikuwa  2,244 sawa na asilimia 0.4,na vyama vingine vyenye usajili wa kudumu walichukua chini ya asilimia 0.1 kwa kila chama.

Hata hivyo waziri Jafo amesema katika zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kulikua na changamoto kwa wagombea wengi kufanya makosa mengi ya kikanuni yaliyopelekea wengi wao kutoteuliwa.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com