Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb)
akijibu swali bungeni leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara
ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeanzisha
mazungumzo na nchi wanachama wa COMESA na nchi kama Misri na Algeria kupitia
balozi zake ili kuandaa Makubaliano Maalum (Bilateral
Agreement) yatakayoiwezesha Tanzania kupeleka tumbaku kwa kodi nafuu.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini
Dodoma leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mhe Edwin Amandus Ngonyani Mbunge wa
Namtumbo aliyetaka kufahamu Wizara ya Kilimo inashirikianaje na Wizara nyingine
zinazohusika na uwekezaji wa mambo ya nje kutafuta soko la tumbaku nchini Misri
badala ya kulazimika kutumia nchi za Uganda na Kenya pekee.
Mazungumzo
hayo yamefikia hatua nzuri na matarajio ni kufungua milango ya soko hilo na
hivyo kuongeza kipato kwa wakulima na taifa kwa ujumla. Aidha, Makubaliano hayo
yakikamilika Tanzania inaweza pia kuuza chai nchini Misri na Algeria kwa faida
kuliko ilivyo hivi sasa au badala ya kuuza chai kupitia mnada wa Mombasa nchini
Kenya.
Mhe
Bashungwa alisema kuwa mwaka 2014/2015 uzalishaji wa tumbaku ya moshi (Dark Fire Cured Tobacco – DFC) ulisimama
mkoani Ruvuma kutokana na kukosa soko.
Hata
hivyo, Jitihada za Serikali ikawezesha Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited (PATL) kuonesha nia ya kununua
tumbaku hiyo ya DFC ambayo nchini Tanzania huzalishwa katika Wilaya ya Namtumbo
na Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.
Alisema
Kampuni hiyo ilieleza kuwa lipo soko kubwa la tumbaku aina ya DFC nchini Misri
na Algeria lakini tumbaku ya Tanzania inauzwa kwa bei ya juu kutokana na kodi inayotozwa
ikilinganishwa na aina hiyo ya tumbaku kutoka nchi za Uganda na Kenya kwa kuwa
nchi hizo (Uganda, Kenya, Algeria na Misri) ni wanachama wa jumuiya ya COMESA
na kwa hiyo kodi za kuingiza tumbaku, chai na bidhaa nchini Algeria na Misri
kutoka Uganda na Kenya ni za chini.
Mhe
Bashungwa alisisitiza kuwa, ili Tanzania iuze tumbaku, chai na bidhaa nyingine
katika nchi za Algeria na Misri kwa faida, inatumia nchi zilizo kwenye jumuiya
hiyo kama Uganda na Kenya.
Kadhalika, Mhe Bashungwa alisema kuwa Wizara ya Kilimo inaendelea kuimarisha masoko ya mazao mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo tayari soko la mahindi limepatiwa ufumbuzi kwa Wizara kuingia mkataba wa mauziano na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuingia mikataba ya masoko ya uhakika kwenye mazao ya kimkakati na mazao mchanganyiko.
Kadhalika, Mhe Bashungwa alisema kuwa Wizara ya Kilimo inaendelea kuimarisha masoko ya mazao mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo tayari soko la mahindi limepatiwa ufumbuzi kwa Wizara kuingia mkataba wa mauziano na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuingia mikataba ya masoko ya uhakika kwenye mazao ya kimkakati na mazao mchanganyiko.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment