METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, September 6, 2020

MGUMBA:ARUDI JIMBONI KUHAKIKISHA CCM INASHINDA



NAIBU waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawana sababu ya kutokipigia Kura chama Cha mapinduzi CCM kutokana Kazi nzuri iliyofanywa na chama hicho kwa kipindi Cha miaka mitano. 

Naibu waziri wa Kilimo Mgumba amebainisha hayo wakati akizungumza katika kikao Cha Halmshauri Kuu Maalum ya   Wilaya ya Morogoro Vijijini,iliyokutana kwaajili ya kuwaleta wanachama wa CCM pamoja ili kuhakikisha chama hicho kinaibuka na ushindi wa kishindo kuanzia udiwani  Ubunge na Urais.

 

Mgumba ambae aligombea kuteuliwa kuwa mbunge la Morogoro Kusini Mashariki na kupata Kura 242, ambapo Hamis Taletale (Babu Tale ) alibuka mshindi na kuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo Hilo na  kwa sasa ni mbunge mteule kutokana na kupita bila kupingwa katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki

 

Omary Mgumba amesema Sasa ni wakati wa kuondosha makundi ya kisiasa kwa kuhakikisha chama Cha Mapinduzi CCM kinapata Ushindi wa kutosha

 

Mgumba pia amesema Innocent Kalogelesi Mbunge Mteule wa Morogoro Kusini  na Hamis Taletale wa Morogoro Kusini Mashariki wananafasi kubwa ya kuhakisha hakuna makundi kwa kuwawake watu kuwa pamoja Mara baada ya kumaliza kwa michakato ya kumpata atakae peperusha bendera katika majimbo ya Morogoro Kusini,na Kusini Mashariki.

 

Katika hatua nyingine amesema kuwa watahakikisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dakta John Magufuli anapata kura za kutosha kutoka majimbo hayo.

 

Amesema kuwa wanaimaani kubwa kuwa majimbo hayo yataongoza kwa kumpigia kura Magufuli kutokana na kile ambacho amekifanya ndani ya Miaka mitano

 

Sanjari na hilo ameongeza kuwa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 imegusa sekta zote muhimu zenye kuja kumkoambo mwananchi.

 

Nao baadhi ya waliokuwa watia nia katika majimbo hayo wameahidi kuungana na walioteuliwa na kuwa kitu kimoja ili kuhakiksha Chama Cha Mapinduzi CCM kinapata kura za kutosha katika majimbo ya Morogoro kusini,na Kusini  Mashariki hasa katika Urais kutokana na tayari kuna wabunge wateule.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com