Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, wakisikiliza maoni, hoja mbalimbali kwenye kikao kazi kilichoshirikisha watumishi wa Wizara hiyo kitengo cha kushughulikia malalamiko ya wananchi Kilicofanyika juzi Mjini Dodoma. (Picha na Veronica Mwafisi-MOHA)
NA VERONICA
MWAFISI, MOHA
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa wito kwa watumishi wa Wizara
hiyo kitengo cha kushughulikia malalamiko ya wananchi, kutekeleza wajibu wao wa
kufuatilia na kuyapatia ufumbuzi wa haraka malalamiko wanayopokea.
Lugola
aliyasema hayo jijini Dodoma juzi katika kikao kazi kilichoshirikisha watumishi
wa kitengo hicho.
Aliwataka
wafuatilie malalamiko yanayotolewa na wananchi dhidi ya taasisi zilizopo chini
ya Wizara hiyo ambazo ni Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Magereza, Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
“Hakikisheni
malalamiko mnayoletewa, mnayapatia ufumbuzi wa haraka bila kufika ngazi ya juu,
tekelezeni wajibu wenu kwa ufanisi ili kujenga imani kwa wananchi
(walalamikaji).
“Kama
wananchi watajiridhisha kuwa kitengo hiki ni msaada mkubwa kwao, mtakuwa
mmejijenga uaminifu na kuifanya Wizara ijitegemee kushughulikia malalamiko,”
alisema.
Lugola
alisisitiza umuhimu wa viongozi wanaoshughulikia malalamiko yanayotolewa na
wananchi kuchukuliwa hatua kama itabainika wameshindwa kutimiza wajibu wao.
Alisisitiza
umuhimu wa kubadili mfumo wa kushughulikia malalamiko akisema yanapofikishwa katika
kitengo hicho yachunguzwe hapo hapo wizarani.
“Malalamiko
yasirudishwe kwenye taasisi zinazolalamikiwa kama Polisi, Uhamiaji, Magereza,
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na NIDA…pia walalamikiwa waitwe na kuhojiwa.
“Lengo
ni kupata suluhisho la malalamiko yanayotolewa ili kuleta uhuru, malalamiko yajibiwe
kwa haraka na uwazikwa njia ya barua ama simu, malalamiko ambayo yataonekana
hayana ukweli walalamikaji wapewe taarifa,” alisisitiza Lugola.
Aliongeza
kuwa, malalamiko mengine hayapaswi kuchukua muda mrefu ili kutatuliwa akitolea
mfano malalamiko ambayo aliyapokea kwa wananchi na kuyapatia ufumbuzi wa haraka
kwenye ziara alizofanya katika mikoa mbalimbali nchini.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, alitumia
fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa kitengo hicho kwa kuyafuatilia malalamiko
yanayotolewa na wananchi pamoja na kuyafanyia kazi kwa haraka.
Alisema
kitendo cha kupokelewa, kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi ndani ya muda
mchache, kitawezekana kama kila mtumishi anayeshughulikia malalamiko
atawajibika ipasavyo ili kupunguza mrundikano wa malalamiko yanayotolewa.
Alitoa
wito kwa watumishi wa kitengo hicho kwenda maeneo mbalimbali ambayo yana malalamiko
ili kupata usahihi wa taarifa, kuzifanyia kazi na kutoa maamuzi.
Kikao
hicho pia kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo na kutoka Jeshi
la Polisi, Magereza, Uhamiaji, NIDA na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment