Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia Zikankuba akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake Kwenye hafla ya kukabidhi mtambo wa kusafisha nafaka uliotolewa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na kuzinduliwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Tarehe 15 Machi 2019.
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma
Kutokana na kukua
kwa Technolojia kila siku, na matumizi ya techolojia yanaongeza ufanisi, Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza na unaendelea na mkakati wa kuhakikisha
kunakuwa na mfumo wa kielektroniki wa kufuatilia na kuhifadhi taarifa za
Hifadhi ya Taifa ya Chakula (Commodity Tracking System).
Lengo la kuwepo
kwa mkakati huo ni kuongeza ufanisi kwa kupunguza mianya ya udanyanyifu na wizi
na ili kufikia lengo hilo ifikapo mwishini mwa mwaka 2020, Mpango wa Chakula
Duniani (WFP) umekubali kusaidia kupata ufadhili wa fedha na utaalamu ili
kufanikisha lengo hilo.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)
Bi Vumilia Zikankuba wakati akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake Kwenye hafla
ya kukabidhi mtambo wa kusafisha nafaka uliotolewa na Mpango wa Chakula Duniani
(WFP) na kuzinduliwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb).
Alisema kuwa WFP
ni mdau muhimu wa NFRA katika kuzungusha akiba ya chakula huku Utekelezaji wa
mauzo ya tani 36,000 ukiwa unaendelea.
Zikankuba alisema
kuwa mpaka sasa Tani zote zimekwisha andaliwa na WFP wamekwisha kuchukua Tani 20,400
huku Tani 15,600 zikiwa zimekwisha andaliwa na zimehifadhiwa vizuri kwa ajili
ya WFP kuchukua.
“Mauzo haya moja
kwa maana yake ni kwamba Mkulima hasa mdogo anapata fursa ya soko la kimataifa
moja kwa moja kwa kuwa NFRA hununua mazao yake moja kwa moja kutoka kwa
wakulima” Alikaririwa
Bi Zikankuba
alitumia mkutano huo kuujulisha ujumbe wa WFP kuwa NFRA ipo tayari na ina uwezo
wa kuuza tani nyingine zaidi baada ya mkataba unaoendelea wa Tani 36,000 kukamilika.
“Pia tupo tayari
kufanya mazungumzo na WFP ili kukusanya na kuwauzia mazao mengine ya nafakai
mtama kuanzia msimu ujao wa mavuno” Alisema
Aliongeza kuwa Mikakati
na programu mbalimbali zinazoendeshwa na WFP zinasaidia NFRA kupata mazao yenye
vigezo kupitia vikundi vya wakulima. Mfano:
Katika msimu huu, kati ya vikundi vya wakulima 216 vilivyouza mahindi yao NFRA
takribani vikundi 62 vilipata mafunzo ya kutunza na huhifadhi mazao ya nafaka
kupitia programu ya Farm to Market Alliance
ya WFP.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment