Leticia Sami (kulia) akitia sahihi katika kiapo chake mbele ya mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) muda mfupi baada ya kula kiapo cha kuwa mjumbe wa baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya Sumbawanga.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. joachim Wangabo (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa baraza la ardhi la Wilaya ya Sumbawanga Bi. Frida Chinuku muda mfupi baada ya hafla ya kiapo cha mmoja wa wajumbe wa baraza hilo.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametahadharisha vitendo vya kuchelewesha
kusikiliza mashauri mbalimbali katika baraza la ardhi na nyumba la Wilaya
ya sumbawanga hali inayowapelekea wananchi kuhisi kuhusisha ucheleweshaji huo
na vitendo vya rushwa na hivyo kuwataka kushikamana na kutafakari kauli mbiu ya
wiki ya sheria yam waka huu iliyowataka kutoa haki kwa wakati kwa kushirikiana
na wadau.
Amesema
kuwa pamoja na mkoa kuwa na baraza moja la wilaya kati ya wilaya zake tatu na
hivyo kupelekea kuelemewa na mashauri yanayotoka katika wilaya nyingine za mkoa
hiyo isiwe sababu ya wajumbe wa baraza hilo kuchelewesha mashauri jambo ambalo
limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu.
“Najua
kuna mzigo mkubwa na mlundikano wa kesi katika baraza, naambiwa kuna mashauri
399 na mengine 36 yamekaa zaidi ya miaka miwili, lakini pamoja na hayo wananchi
nao wanlalamika kuhusiana na baraza la ardhi na nyumba Sumbawanga, moja ya
malalamiko makubwa ni kwamba mashauri yanachelewesha ambapo wanachi wanaona
kuna mashauri mengine yasingepaswa kuchukua muda mrefu na hili linaungana na
lalamiko la pili ambalo linahusishwa baraza hili na vitendo vya Rushwa,” Alisema.
Ameyasema
hayo katika hafla fupi ya kumuapisha mjumbe wa baraza la ardhi na nyumba la
wilaya ya Sumbawanga Bi. Leticia Sami, ambapo kwa sasa Mkoa wa rukwa una baraza
moja tu la ardhi na nyumba ambalo linapatikana katika wilya ya Sumbawanga.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Sumbawanga Bi.
Frida Hamis Chinuku alisema kuwa mchakato wa kumpata mjumbe huo unaanzia kwa
majina kupendekezwa na Mkuu wa Mkoa na kisha majina hayo kupelekwa kwa Waziri
mwenye dhamana ambapo humteua mjumbe na hatimae mjumbe huyo kuapishwa.
“Mjumbe
yeyote kabla ya kuanza kazi anatakiwa kuapishwa na Mkuu wa mkoa katika Mkoa
husika ambako baraza lipo, mchakato wa kumpata mjumbe huyu ulianza mwaka jana
2018 na aliteuliwa rasmi tarehe 5. July mwaka 2018 na kuapishwa leo. Kwa sasa
baraza litakuwa na wajumbe jumla wanne japokuwa mjumbe mmoja ni mgonjwa,”
Alisema.
Kiapo
hicho kinatokana na maelekezo ya Kanuni za mwaka 2003 za Sheria ya namnba 2 ya
utatuzi wa migogoro ya ardhi ya mwaka 2002.
0 comments:
Post a Comment