Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani humo katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) aizungumza na Meneja wa Wanachama kutoka NHIF(kushoto) na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Benard Konga, mara baada ya kumalizika kwa Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa Serikali na viongozi wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)mkoani Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yakiwasilishwa katika Jukwaa la Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wanavyoweza kujiunga na Bima ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika Machi 14, mjini Bariadi.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema
mkoa huo umejiwekea malengo ya kuhakikisha zaidi ya asilimia 80 ya wananchi
wake kuwa na kadi za bima ya afya ili kujihakikishia upatikanaji wa
huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini.
Mtaka ameyasema hayo wakati ufunguzi wa Jukwaa la
Ushirika Afya Mkoa wa Simiyu lililofanyika kwa lengo la kujadili namna
wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS)wanavyoweza kujiunga na Bima
ya afya na kupewa kadi kupitia vyama vyao na kama familia, ambalo limefanyika
Machi 14, mjini Bariadi.
Amesema yeye kama Mkuu wa Mkoa atafanya vikao na
wanachama wa AMCOS na makundi mbalimbali ya wananchi katika wilaya zote
mkoani hapa na kuzungumza nao kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kila mwananchi
kuwa na Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu.
Aidha, amesema atawaelimisha wananchi juu ya
umuhimu wa kuwa katika Vyama vya Ushirika Vya Msingi ambavyo vinawapa nafasi ya
kupata Bima ya afya na kupata matibabu makubwa katika vituo vya kutolea huduma
za afya vya binafsi na vya umma kwa gharama nafuu ya shilingi 76,800/= kwa mtu
mmoja(mwanachama wa ushirika).
“Nitafanya vikao na wanachama wa AMCOS zote,
wakulima, wafugaji, wajasiriamali, makundi yote ya wananchi kwenye mkoa wetu wa
Simiyu, tuweze kuwaelimisha faida ya mwananchi wa mkoa wa Simiyu kuwa na bima
ya afya, kubwa zaidi umuhimu wa kuwa kwenye ushirika ambao utamwezesha kupata
matibabu makubwa kwa bei nafuu” alisema
Katika hatua nyingine Mtaka amesema katika kipindi
cha msimu wa pamba kila kituo cha kununulia pamba NHIF itaweka Afisa wake kwa
ajili ya kusajili wakulima na wanachama wa vyama vya ushirika walio tayari,
hivyo akatoa wito kwa viongozi walioshiriki jukwaa la ushirika afya kutoa
taarifa na elimu kwa wenzao juu ya umuhimu wa suala hilo.
Mtaka pia ametoa wito kwa wakulima wote wa pamba
kulipa kipaumbele suala la afya kwa kuchukua hatua ya kuwa na bima za afya ili
waweze kuona manufaa ya Serikali kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na
kujenga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Hospitali za wilaya kwa kila wilaya na
Vituo vingine vya kutolea huduma za afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernad Konga amesema NHIF ni
wadau wakubwa mkoani Simiyu, hivyo wako tayari kutoa huduma bora na watawafikia
wananchi wa makundi yote mkoani hapa na watahakikisha wanatoa kadi za bima ya
afya kwa wakati kwa wanachama wote watakaojiunga.
Katika jukwaa hili washiriki wamepata
nafasi ya kuchangia michango mbalimbali huku wanachama wa AMCOS wakiunga mkono
mpango huo wa kupata bima ya afya kwa gharama ya shilingi 76,800/= ili waweze
kumudu gharama za matibabu.
“Mpango huu nimeupokea vizuri ila ninashauri
elimu iendelee kutolewa zaidi na zaidi ili wanachama wote wajue umuhimu wa kuwa
na kadi za bima ya afya na namna zitakavyowasaidia” Lucas Ephraim mshiriki
kutoka AMCOS ya Dutwa Bariadi.
“ Binafsi niko tayari kujiunga na mfuko wa
bima ya afya ili nipate hiyo kadi itakayonifanya niweze kutibiwa popote hapa
Tanzania, lakini naomba tutakapolipia hiyo 76,800/= kadi zetu tuzipate mapema”
Mmoja wa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya msingi, Bw. Magwashi Gandila
Mkoa wa Simiyu una vyama vya Ushirika Vya
Msingi(AMCOS) zaidi ya 379 vyenye wanachama zaidi ya 300,000 na Jukwaa hili
limeazimia wanachama wa AMCOS wakawe mabalozi wazuri kuwahamasisha
wananchi kujiunga na Bima ya Afya.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment