METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, July 31, 2017

WANANCHI WA MKOA WA RUKWA KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASILIAMALI YA SIKU TATU

Na: Ramadhani Shabani

Ndugu Mtanzania Ni Tumaini Langu Wewe Ni Buheri Wa Afya Na Unaendelea Vyema Na Utekelezaji Wa Kauli Mbiu Ya Hapa Kazi Tu!Ikiwa Imelenga Kunyanyua Kipato Cha Mtanzania Wa Chini Na Kuipaisha Nchi Yetu Kufikia Kuwa Nchi Ambayo Watu Wake Wanavipato Vya Uchumi Wa Kati.

Ndugu Mtanzania Kama Kawaida Yetu Ya Kukuletea Taarifa Mbalimbali Zinazoendana Na Kasi Ya Ya Utekelezaji Wa Kauli Mbiu Ya Hapa Kazi Tu!Na Leo Hii Nimekuletea Hii Taarifa Moja Kwa Moja Kutoka Wilaya Ya Sumbawanga Mjini Mkoani Rukwa,.

Ndugu Mtanzania Taarifa Hii Inahusu Mafunzo Ya Ujasiliamali Ambayo Yamepata Udhamini Kutoka Kwa Mbunge Wa Viti Maalum CCM Mkoa Wa Rukwa *Mhe Bupe Nelson Mwakangata*Huku Yakifunguliwa Na Mwenyekiti Wa Vijana (UVCCM) Wa Wilaya Ya Sumbawanga Mjini Ndugu *Andrew Matanila*.

Akifungua Mafunzo Hayo Ya Ujasiliamali Mwenyekiti Wa Vijana Wa Wilaya Ya Sumbawanga Mjini Ndugu *Andrew Matanila*Alisema Mafunzo Hayo Yaliyofunguliwa Leo Yatadumu Kwa Muda Wa Siku Tatu Yani Kuanzia Leo Jumatatu Na Kufungwa Siku Ya Jumatano Na Mdhamini Mkuu *Mhe Mbunge Wa Viti Maalum Mkoa Wa Rukwa Ndugu Bupe Nelson Mwakangata* Ambaye Ndiye Aliyegharamia Gharama Zote Na Kuwaleta Wakufunzi Hao Kwa Ajili Ya Hayo Mafunzo Ya Ujasiliamali.

Mafunzo Hayo Yanayoendelea Ktk Viwanja Vya Nelson Mandela Yamejikita Ktk Kumsaidia Mwananchi Wa Rukwa Na Haswa Kwa Sumbawanga Mjini Ambako Ndio Tayari Yanatolewa Kujikwamuwa Na Umasikini Kwa Kumpa Maarifa Ya Kufanya Shughuli Mbalimbali Ambazo Haziitaji Gharama Kubwa Ya Mitaji Mfano,

1.)Kufanya Kilimo Bora Na Cha Kisasa.
2.)Ufugaji Bora Na Wakisasa.Ikiwemo Ufugaji Wa Kuku Wa Nyama Na Wa Mayai Kwa Muda Wa Miezi Mitatu.
3.)Kutengeneza Bidhaa Mbalimbali Za Viwandani Mfano,Sabuni Ya Maji,Sabuni Ya Unga,Sabuni Ya Alovela,Sabuni Ya Majivu,Sabuni Ya Magadi.
4.)Lakini Pia Bila Ya Kusahau Namna Ya Kutengeneza Batiki,Vikoi pamoja Na Vitenge.

Akifungua Mafunzo Hayo Ambayo Yapo Chini Ya Udhamini Ya Mbunge Wa Viti Maalum Mkoa Wa Rukwa *Mhe Bupe Nelson Mwakangata* Mwenyekiti Wa Vijana Wa Wilaya Ya Sumbawanga Mjini Ndugu Andrew Matanila Alimpongeza Sana Mbunge Huyu Kwa Kusema Kwamba Ni Mbunge Makini Na Mzalendo Aliyelenga Kweli Kuwatumikia Wananchi Wa Mkoa Wa Rukwa Kwa Nafasi Yake Ya Ubunge Aliopewa Huku Akiwataka Wananchi Wa Mkoa Wa Rukwa Na Hasa Vijana Kujitokeza Kwa Wingi Zaidi Kumuunga Mkono Mbunge Huyo Kwa Kuakikisha Wanapata Mafunzo Hayo Ya Ujasiliamali Na Kuyatumia Vizuri Iliwaweze Kujikwamuwa Na Umasikini,Lakini Pia Aliwataka Vijana Baada Ya Kuyapata Mafunzo Hayo Ya Ujasiliamali Kwenda Na Kujiunga Na Vikundi Mbali Mbalimbali Vya Ujasiliamali Kwani Yeye Kama Mwenyekiti Wa Vijana Yupo Tayari Pia Kuakikisha Vijana Wananufaika Na Mafunzo Hayo Ya Ujasiliamali Yanayotolewa Na *Mhe Bupe Mwakangata* Kwa Kuakikisha Kwamba Sasa Anaungana Kwa Dhati Na Ndugu Kaimu Katibu Mkuu Wa Vijana Taifa *Shaka Hamdu Shaka* Ktk Kuakikisha Fungu La Asilimia Tano Linatolewa Kwa Ajili Ya Vijana Ili Kuweza Kukopeshwa Na Kutumia Fedha Hizo Kama Mitaji Ktk Kuenzi Mafunzo Hayo Ya Ujasiliamali.

CCM Mpya Na Tanzania Mpya Ni Matokeo Chanya Na Taraji Kwa Kila Mtanzania

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com