Na
Issa Mtuwa Dodoma
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara ya Madini kwa
utekelezaji wa Ujenzi wa Jengo la Taaluma la chuo cha Madini Dodoma (MRI) na
Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Wizara ya Madini lilipo eneo la Mji wa Serikali
Ihumwa, Jijini Dodoma.
Hayo
yamesemwa Machi 13, 2019 na Wajumbe wa Kamati
hiyo wakati wa kikao cha majumuhisho kilichofanyika kwenye jengo la wizara ya Madini
Ihumwa, mara baada ya kukagua majengo yote mawili na kupewa taarifa ya ujenzi
wake.
Wakiwa
kwenye jengo la taaluma la chuo cha madini, wajumbe wamepongeza na kuridhishwa
na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na
kupongeza SUMA JKT kujenge jengo hilo.
Jengo
la Taaluma ni la ghorofa tatu lenye ofisi, vyumba vya kufundishia na ukumbi wa
mikutano. Ujenzi huo utagharimu jumla ya shilingi 2, 863, 161, 369.00 hadi
kukamilika kwake na unatekelezwa chini
ya chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Raslimali Madini (SMMRP) kwa mkopo
kutoka Benki ya Dunia.
Akizungumzia
ujenzi wa jengo la Wizara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila
amewaeleza wajumbe wa kamati kuwa, ujenzi huo ulianza tarehe 4/12/2018 na
ulitakiwa kukamilika tarehe 31/01/2019, hata hivyo mkandarasi hakuweza
kukamilisha ndani ya muda huo kutokana na sababu mbalimbali. Prof. Msanjila
ameongeza kuwa, kwa kuzingatia ushauri wa msimamizi wa ujenzi huo, walifikia
makubaliano ya kumuongezea muda mkandarasi hadi kufikia tarehe 28/02/2019.
Prof.
Msanjila ameongeza kuwa, mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 80 na mwezi
ujao wizara itakuwa tayari kuhamia. Amesema ujenzi huo umegharimu Jumla ya
shilingi Milioni 975,360,028.10 zitatumika katika ujenzi huo.
Naye, Waziri wa Madini Doto Biteko ameiambia
kamati kuwa, mkandarasi wa ujenzi huo, alipewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha
ujenzi wake ili wafanyakazi wa Wizara hiyo waanze kulitumia. Waziri emeleza
kuwa wizara inaridhishwa na kasi ya mkandarasi katika ujenzi huo.
Biteko
ameongeza kuwa, wizara imedhamiria kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati
na kuthibitisha hilo wizara imemteuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na
Raslimaliwatu, Nsajigwa Kabigi ambae yupo muda wote wote eneo la ujenzi.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dunstan Kitandula amesema pamoja na
wabunge kuipongeza wizara kwa kazi nzuri, ameishauri wizara na mkandarasi wa
ujenzi huo, Mzinga Holdings Company kujielekeza kwenye manunuzi ya vifaa
vinavyopatikana hapa nchini.
Wakichangia
wajumbe wa kamati hiyo, Joseph Musukuma na Ally Keissy wakichangia wakati wa
majumuhisho waliipongeza wizara na mkandarasi, hata hivyo, walishangaa muda
waliopewa na hatua iliyofikia, msukuma alisema ni kazi ya kupongeza na wameeleza pamoja na mkandarasi kutokamilisha
kazi yake kwa wakati bado utendaji wake wa kazi unaridhisha na kasi yake inaonekana.
Naye,
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo aliwaambia wajumbe wa kamati kuwa,
ujenzi wa jengo hilo la wizara unafanana ramani na wizara nyingine ikiwemo
kiasi cha fedha zilizotolewa na serikali zote zikiwa na kiwango cha shilingi
Bilioni moja.
Amesema
muda uliotolewa ulilenga kutimiza azma ya wizara kuhamia eneo hilo kwa wakati.
Aliwashukuru wajumbe kwa ushauri wao na kueleza kwamba kama wizara watauzingatia.
0 comments:
Post a Comment