METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, February 13, 2019

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA DERNMARK NCHINI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akisalimiana na Balozi wa Denmark Nchini Einar Jensen walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake Februari 13, 2019 Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza jambo na balozi wa Denmark Einar Jensen alipokutana naye kuzungumza masuala ya uwekezaji nchini, Februari 13, 2019 Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika  picha ya pamoja na  Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen pamoja na wageni alioambatana  nao  mara baada ya kikao hicho.
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Dernmark nchini Einar Jensen juu ya masuala ya maboresho ya mazingira ya biashara pamoja na uwekezaji nchini.
Mazungumzo hayo yamefanyika hii leo Februari 13, 2019 katika Ofisi yake Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kuona namna bora ya kuimarisha masuala ya uwekezaji nchini kwa kuzingatia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Alimtaka balozi kuendelea kuona fursa na kuzitumia hususan katika kuwekeza kwenye viwanda hasa vya nguo, mazao ya biashara pamoja na kilimo kwa kuwa ndiyo maeneo yenye fursa nyingi pamoja na kuleta chachu ya ukuaji wa viwanda nchini.
“Ni vizuri kuendelea kuimarisha mazingira ya biashara ili kuendelea kuvutia wawekezaji hasa maeneo ya kilimo na viwanda vya nguo kwa kuwa vinatija katika ukuaji wa uchumi,”Alisitiza Kairuki
Aidha aliendelea kumpongeza balozi huyo kwa kutumia muda wake kumtembelea ofisi kwake kwa lengo la kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masula ya kuboresha mazingira ya biashara pamoja na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.
“Kipekee nikushukiuru  kwa kutembelea ofisi yetu na hii ni ishara nzuri yakuimarisha mahusiano  ya kidiplomasia ambayo yatasaidia Serikali yetu kuendelea kuwa na mazingira rafiki kwa wawekezaji  kuzingatia fursa zilizopo katika maeneo mengi ikiwemo; Sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini”alisisitiza kairuki
Kwa upande wake Balozi wa Dernmark nchini, Einar Jensen aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika maeneo ya maboresho ya biashara ikiwa ni pamoja na kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali
“Nimefarijika kukutana na Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji na kupata muongozo wa masuala ya uwekezaji nchini na kuendelea kutumia fursa zilizopo Tanzania na ninaahidi kutoa ushirikiano ili kuleta chachu katika ukuaji wa viwanda kwa kuleta wawekezaji katika sekta mbalimbali,”alisistiza Jensen.
=MWISHO=
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com