Mgeni Rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza ushirikiano wa serikali kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo wakati akifungua mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha, leo tarehe 25 Februari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya washiriki wakifatilia mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha, leo tarehe 25 Februari 2019.
Mgeni Rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati akifungua mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha, leo tarehe 25 Februari 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Daqarro akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha, leo tarehe 25 Februari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha, leo tarehe 25 Februari 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya kilimo-Arusha
Serikali imeeleza
kuwa imejipanga kuweka mazingira wezeshi katika kutekeleza Mradi wa uendelezaji
na upatikanaji wa mbegu za mazao jamii ya mikunde na nafaka Afrika (The Accelerated
Varietal Improvement and Seed Delivery of Legumes and Cereals in Africa
project-AVISA). utakaosimamiwa na
kutekelezwa kwa ukamilifu nchini Tanzania.
Waziri wa Kilimo
Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 25 Februari 2019 wakati
akifungua mkutano wa Mradi wa uendelezaji na upatikanaji wa mbegu za mazao
jamii ya mikunde na nafaka Afrika (AVISA) uliofanyika katika ukumbi wa Mount
Meru Hotel Jijini Arusha.
Katika ufunguzi
huo wa mkutano wa siku tatu, Mhe Hasunga alisema kuwa ana mategemeo makubwa
kuwa katika mradi huo msukumo mkubwa utawekwa katika uhaulishaji wa teknolojia
kupitia uimarishaji wa mashirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili
matokeo ya mradi yaweze kuonekana kwa walengwa.
Alisema, Kilimo
kimeendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi katika nchi nyingi za Afrika ikiwemo
Tanzania. “Kwa mfano, hapa Tanzania kilimo kinachangia asilimia 29.1 katika
pato la taifa na karibia asilimia 65.5 ya nguvu kazi inategemea kilimo”
“Hata hivyo, kwa
Afrika kilimo kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukame,
upungufu kwa rutuba katika udongo, kuongezeka kwa magonjwa na wadudu wa mazao
vipando, miundombinu hafifu, kipato kidogo kwa wakulima, upokeaji mdogo wa
teknolojia, soko lisilokuwa la uhakika na bei ndogo za mazao, kutegemea kilimo
cha jembe la kutumia mkono na mifumo hafifu ya uzalishaji na usambazaji wa
mbegu bora. Hivyo, hali hii inasababisha uzalishaji mdogo, ubora mdogo wa mazao
na kuwafanya wakulima kubakia kuwa wadogo na kulima kwa kujikimu tu sio
kibiashara” Alikaririwa Mhe Hasunga
Alisema kuwa, ana matumaini makubwa kuwa Mradi huo utaimarisha
mafanikio yaliyopatikana kutoka kwenye miradi ya utafiti iliyotangulia ya
Mikunde (Tropical Legumes -TL), Uendelezaji wa Tija katika Mazao ya Mtama
na Ulezi (Harnessing Opportunities for Productivity Enhancement for Sorghum and
Millets - HOPE) na Harvest Plus ambayo ilifadhiliwa na
Shirika la Bill & Melinda Gates Foundation (BMGF) – kwa ajili ya kuendeleza
uzalishaji wa mbegu na usambazaji wake.
Aidha, BMGF imekuwa ikifadhili miradi hiyo katika nchi saba (7) za Afrika
zikiwemo Tanzania, Uganda, Ethiopia, Burkina Faso, Ghana, Mali na Nigeria
katika utafiti wa dengu, karanga,
maharagwe, kunde, mtama na ulezi. Hivyo, Mradi huo wa AVISA utaendeleza na
kuimarisha mashirikiano kati ya Vituo vya
Kimataifa vya Utafiti wa Kilimo (CGIAR) na Mifumo ya Kitaifa ya Utafiti
wa Kilimo katika nchi za Afrika (NARS) katika kuendeleza uzalishaji na
usambazaji wa mbegu za aina ya nafaka na mikunde zinazohimili maeneo ya
ikologia ya ukame.
Manufaa mengine
ni kuimarisha na kuongeza madini ya chuma na zinki katika mazao ya maharagwe na
ulezi katika mradi wa HarvestPlus unaofadhiliwa na BMGF kupitia CIAT (Maharage)
na ICRISAT (Ulezi). Hivyo, kuwekeza Miradi miwili ya TL-III na HOPE ambapo itaongeza
tija kwenye mazao husika na kujenga
uwezo wa utafiti kwenye nchi zetu za Afrika.
Mkutano huo
ulihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Daqarro, Wawakilishi
Shirika la Bill & Mellinda Gates, likiongozwa na Dkt Jeff Ehlers, Mkurugenzi Mkuu ICRISAT: Dkt Peter Carberry, Wakurugenzi wa Taasisi za Utafiti za Kanda: CIAT, ICRISAT and IITA, Wawakilishi wa Shirika la Syngenta, Wakurugenzi Wakuu, Taasisi za Utafiti wa Kilimo kutoka: Uganda,
Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Mali and Tanzania, Wakurugenzi wa Wizara ya Kilimo na Wakuu wa Taasisi zake Wawakilishi wa Makampuni ya Mbegu, Wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya Serikali pamoja na Wawakilishi wa Vyama vya Wakulima.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment