Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akitoa maelezo kuhusu vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo kwa wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Saza Wilayani Songwe
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akimpatia kitambulisho cha wajasiriamali wadogo wadogo mchimbaji mdogo wa madini katika Kijiji cha Saza Wilayani Songwe
Afisa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato nchini TRA Omary Iddi akitoa maelezo kuhusu vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo kwa wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Saza Wilayani Songwe
Baadhi ya wajasiriamali wadogo wadogo wakipata maelezo na wengine wakichukua vitambulisho vya wajasiriamali katika eneo la Mkwajuni Wilayani Songwe.
Wavuvi na wachimba madini
wadogowadogo wamepewa muda wa siku nane kuchukua vitambulisho vitakavyo
wawezesha kutambulika rasmi kama wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kufanya
shughuli halali za uzalishaji mali bila kusumbuliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
(Mst) Nicodemus Mwangela ametoa maelekezo hayo mapema wiki hii akiwa ziarani
Wilayani Songwe ambapo ametembelea kambi ya wachimbaji wadogo wa madini katika
Kijiji cha Saza na wajasiriamali wa uvuvi katika kambi ya sabasaba pembezoni
mwa mto Rukwa.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela amesema,
“mjasiriamali mdogomdogo unayefanya shughuli yeyote halali inayokuingizia
kipato na hulipi kodi TRA serikali inataka kukutambua hivyo basi unatakiwa
kuchukua kitambulisho ili usisumbuliwe”.
Aidha amezitaka halmashauri za Mkoa
wa Songwe kuhakikisha zinasimamia vizuri ugawaji wa vitambulisho vya
wajasiriamali wadogo ili kuepuka udanganyifu na kuhakikisha kila mjasirimali
anatambulika kwa kupata kitamblisho hicho.
Naye Afisa Kodi Kutoka Mamlaka ya
Mapato nchini TRA Omary Iddi amesema wajasiriamali wadogowadogo ambao kipato
chao kwa siku wanapata chini ya shilingi milioni nne kwa mwaka wanapaswa
kuchukua kiambulisho cha Ujasiriamali ili nao waweze kuchang pato la taifa.
Wajasiriamali wadogo wanaoishi kwenye
kambi ya uvuvi ya Sabasaba, Wachimbaji wadogo wa madini wa Saza na
wajasiriamali wegine Wilayani Songwe wamezipongeza juhudi za serikali za kuweka
mazingira mazuri ya ulipaji kodi kwa manufaa ya maendeleo ya Taifa.
Simkonda Maiko amesema anaipongeza
serikali kwa kuwatambua wajasiriamali wadogo wadogo na hivyo kuwawekea
utaratibu mzuri wa kuchangia mapato pia itawasaidia kutosumbuliwa.
0 comments:
Post a Comment