Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika akizungumza wakati wa Kikao cha Mawaziri Saba wakioongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kujadili changamoto za sekta ya ardhi nchini.Kikao kimefanyika Ofisi za TAMISEMI Dodoma leo tarehe 7 Februari 2019.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika akizungumza wakati wa Kikao cha Mawaziri Saba wakioongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kujadili changamoto za sekta ya ardhi nchini.Kikao kimefanyika Ofisi za TAMISEMI Dodoma leo tarehe 7 Februari 2019.
Na Munir Shemweta, Dodoma
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi leo
tarehe 7 Februari 2019 ameongoza kikao cha Mawaziri wenzake sita kujadili
changamoto mbalimbali za matumizi ya sekta ya ardhi.
Mkutano huo unaohusisha pia Makatibu Wakuu wa Wizara hizo
unafuatia maagizo yaliyotolewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Pombe Magufuli januari 15, 2019 kwa wizara hizo kukutana na kushughulikia
changamoto katika matumizi ya sekta ya ardhi kwa nia ya kutatua migogoro.
Mawaziri wanaoshiriki kikao hicho ni kutoka Wizara ya Maliasili na
Utaliii, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya
Maji, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Muungano (Mazingira) pamoja na ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kikao hicho cha Mawaziri kimetanguliwa na mfululilizo wa vikao vya
timu ya wataalamu kutoka wizara hizo ikioongozwa na Kamishna wa Ardhi nchini
Marry Makondo kwa nia ya kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi ambayo imekuwa
ikijotokeza katika maeneo mbalimbali nchini.
Muendelezo wa vikao vya aina hiyo ni jitihada za Rais John Pombe
Magufuli kuhakikisha migogoro ya ardhi nchini inapungua kama siyo kuisha kabisa
na hivyo kuleta faraja kwa wananchi wanaoishi maeneo yenye migogoro ambao
wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi.
Januari 2019 Mawaziri watano wakioongozwa na Waziri wa nchi ofisi
ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo walikutana mkoani Kigoma kujadili changamoto
katika Hifadhi za Misitu na Mapori ya Akiba ya Moyowosi mkoani Kigoma. Hifadhi
hiyo imekuwa na mgogoro kwa muda mrefu kutokana na wananchi kuendesha shughuli za
kiuchumi katika hifadhi hizo.
----------------------------- MWISHO------------------------ ------------------------------ --------------
0 comments:
Post a Comment