Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na Wadau wa Sekta Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo Tarehe 12 Februari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba (Mb) akizungumza wakati wa mkutano na Wadau wa Sekta Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo Tarehe 12 Februari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na Wadau wa Sekta Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo Tarehe 12 Februari 2019.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza wakati wa mkutano na Wadau wa Sekta Binafsi uliofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo Tarehe 12 Februari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano na Wadau wa Sekta Binafsi mara baada ya kufungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo Tarehe 12 Februari 2019.
Serikali
imesema kuanzia sasa haitatoa vibali vya uagizaji sukari nje ya nchi kwa
wazalishaji wa sukari badala yake serikali itatafuta utaratibu mwingine wa
kuagiza.
Waziri
wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 12 februari 2019 wakati
akifungua mkutano na Wadau wa Sekta Binafsi ambapo; lengo lilikuwa ni
kubadilishana uzoefu, kupata maoni yao namna bora ya kuongeza mahusiano pamoja
na utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP II) ambayo
inatekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali na Sekta Binafsi.
Waziri
Hasunga imewataka wazalishaji hao wa sukari nchini kuja na mkakati wa namna
gani wataongeza uzalishaji ili Tanzania iondoke na hitaji la kuagiza bidhaa
hiyo nje ya nchi.
Waziri
Hasunga amesema kwa kuwapa vibali vya kuagiza nje wazalishaji wa ndani
hawataongeza uzalishaji ili waendelee kuagiza nje kwa kuwa sukari ya kutoka nje
ni bei nafuu.
"Wazalishaji
wa ndani ndio hao hao wanapewa vibali vya kuagiza, umewahi sikia wapi?
Wataongeza ukweli kasi ya uzalishaji? Na Mimi niwaambie kabisa hilo hapa kwangu
halipo kabisa kama ni kuagiza nitaagiza mimi," alisema Waziri Hasunga.
Amesema
mahitaji la sukari kwa mwaka ni Tani 670,000 wakati inayozalishwa na viwanda
vya ndani Tani 320,000 na kuwaagiza Wazalishaji hao badala ya kutafuta vibali
vya kuagiza sukari nje ya nchi waje na mkakati wa kuboresha zaidi uhitaji
uliopo kwani Tanzania ina ardhi nzuri pamoja na mashamba ya kutosha.
"Kama
kuna Wafanyabiashara ambao walikuwa wanasubiri baada ya kikao hiki waje kuomba
vibali wasahau kabisa, kwangu halipo badala yake nina mkakati wa kuboresha
uzalishaji ili tusiagize tena nje," alisema Waziri Hasunga.
Amesema
kuwa anataka kuhakikisha ndani ya miaka mitatu Tanzania haitaagiza sukari nje
tena kwa kujitosheleza kwa kilimo cha miwa na kukaribisha wawekezaji kujenga
viwanda vya kutengeneza sukari, "kama tutakunywa kwa chumvi sawa, hapo
ndio tutafanya bidii."
Waziri
Hasunga amesema hayuko tayari kuondoshwa kazini kwa utoaji wa vibali vya sukari
kwa Wafanyabiashara wanaoagiza nje ya nchi kwani anaamini kuwa uwezo wa
kuzalishwa hapa nchini upo. Waziri huyo alisema serikali inatoa fedha nyingi
kuagiza bidhaa za chakula kutoka nje.
Alisema
kwa mwaka zaidi ya Shilingi Bilioni 400 zinatumika kuagiza mafuta nje ya nchi
wakati kuna uwezo wa kulima mazao mbalimbali yanayozalisha mafuta ikiwa ni
pamoja na michikichi.
"Mimi
naamini katika nchi zilizobarikiwa na kupendelewa ni pamoja na Tanzania, ardhi
yenye rutuba, mito mingi na mbuga za wanyama lakini watu hawalimi kilimo cha
umwagiliaji," alisema.
Ameitaka
Sekta Binafsi kuhakikisha kunakuwa na mashamba makubwa ambayo yatazalisha mazao
yanayohitajika kwa viwanda na pia mazao ya chakula.
Waziri
Hasunga amewataka Wadau wa Sekta Binafsi kutumia kikao hicho kutoa maoni,
mapendekezo yenye muelekeo wa kutatua changamoto katika Sekta ya Kilimo ambapo
anategemea maboresho hayo yataleta mabadiliko makubwa katika mfumo mzima wa
pembejeo za kilimo, masoko, uzalishaji wenye tija na utungwaji wa sheria ya
kilimo.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment