Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya
Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu
jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Ummam, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jiji Dar es salaam, Januari 24, 2019. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula, Mjumbe wa Bodi, George Mlawa na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, George Mlawa baada ya mazungumzo na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi
ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa
weledi.
Ameiagiza
ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi, akitolea
mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na kazi
wanazozifanya.
Amekutana
na wajumbe wa bodi hiyo leo (Alhamisi,Januari 24, 2019) katika kikao
kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi ya
watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bodi hiyo ifanye kazi
kwa bidii.
Amesema
Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini sahihi
ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kuboresha utendaji wa watumishi wa
umma nchini.
Serikali
inaimani kubwa na wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao
kwenye utumishi wa umma.
“Tunataka
muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa waledi bila
ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na kupokea rushwa.”
Amesema
Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika kuwatumikia
wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na upatikanaji wa maslahi
mazuri.
0 comments:
Post a Comment