Kesi nyingi
zinazoripotiwa kwa sasa katika madawati ya jinsia na watoto zimebainisha kuwa
watu wengi wamekuwa wakijifanyia ukatili pasipo wenyewe kujijua.
Hayo
yameelezwa mapema jana jijini Dar es salaam na Afande Christina Onyango ambaye ni
Mratibu wa Dawati la jinsia na watoto Mkoa wa Kipolisi Ilala katika muendelezo wa kampeni ya kupinga
rushwa ya ngono katika mkoa huo.
Afande huyo
alisema watu wengi wamekuwa wakitoa rushwa ya ngono bila kujua kuwa
wanalolifanya ni kosa kisheria kwa mtendaji na hata mtendewa Kwa kuwa
inahesabiwa ni rushwa kama rushwa nyingine.
Aliongezea
kuwa kitendo hicho kinaleta madhara makubwa katika jamii ikiwemo kushusha hadhi
ya mtu, kufanya kazi kwa woga na hata kusababisha kupata magonjwa ya zinaa kama
gono na ukimwi.
Aliendelea
kusema kuwa program hiyo ilianza rasmi kwenye siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia na mpaka sasa haina mfadili wa kudumu ila kwa hii ya leo imefadhiliwa
na Women Fund kwa kushirikiana na Dawati ya jinsia na watoto mkoa wa Kipolisi
Ilala.
Katika Mdaharo
huo uliofanyika katika kata ya Vingunguti jijini Dar es salaam huku Mgeni Rasmi
akiwa ni Adam Maru ambaye ni OCD wa Buguruni , wamesema kuwa lengo ni kuzifikia
kata zote za Mkoa wa Kipolisi Ilala ili wananchi wafahamu madhara ya rushwa ya
ngono ndani ya jamii yao.
Kwa upande
wake Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Buguruni OCD Adam Maru alisema kesi
nyingi wanazozipokea ni za ukatili wa majumbani hasa kwa watoto, wanawake
lakini pia hata wanandoa kufanyiana ukatili wenyewe kwa wenyewe.
Aliongeza
kuwa kesi hizi kwa sasa zimepungua na hii ni kutokana na kuwepo kwa elimu kubwa
inayotolewa pamoja na uwepo wa madawati katika vituo vya polisi, kwa kuwa hapo
mwanzo watu walikuwa wakibaki na machungu yao moyoni bila kufahamu wapi ni
mahali sahii pa kuyapeleka.
Aidha Kamanda
Adam amewataka wananchi kuweza kuvunja
ukimya na kuamua kufunguka juu ya ukatili wa kijinsia na kuacha tabia ya
kuficha mambo kwa kuhofia mtendaji wa ukatili hata akiwa ni ndugu wa karibu
aidha mjomba, kaka hata baba mdogo na kuamua kumripoti katika dawati la Jinsia.
Kikundi cha Milembe Joging kikiwasili katika viwanja vya Vingunguti Machinjioni mapema jana jijini Dar es salaam, katika Mdaharo wa kupinga Rushwa ya Ngono.
Afande Christina Onyango ambaye ni Mratibu wa Dawati la jinsia na watoto Mkoa wa Kipolisi Ilala akiongea na wakazi wa vingunguti katika Mdaharo ulioandaliwa na Dawati la jinsia mkoa huo.
Inspekta Lydia kutoka Dawati la jinsia Chanika akimkaribisha Mgeni Rasmi ambaye ni Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Buguruni.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Buguruni OCD Adam Maru akiongea na wakazi wa kata ya vingunguti juu ya changamoto ya Rushwa ya Ngono hapa nchini.
Naibu Meya wa Ilala ambaye pia ni Diwani wa Vingunguti Bw. Omary Kumbilamoto akiwasalimia wakazi wa kata hiyo.
Meza kuu ikiwa katika majadiliano.
Wakazi wa Vingunguti na maeneo ya karibu wakifuatilia Mdaharo ulioandaliwa na Dawati la Jinsia mkoa wa Kipolisi Ilala.
0 comments:
Post a Comment