Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mzee Eric Mchata. Kulia aliyekaa ni Meneja Maendeleo, Utawala na RasilimaliWatu wa kampuni ya Mantra Tanzania, Phillemon Tano.
Sehemu ya Wataalam wa wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini wakifuatilia kikao cha kusuluhisha mgogoro kati ya kampuni ya Mantra na Mzee Eric Mchata. Kutoka kulia ni Kamishna wa Tume ya Madini, Prof. Abdulkarim Mruma, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Afisa Sheria wa Wizara ya Madini, Joseph Nyamsenda.
Waziri
wa Madini, Doto Biteko leo Januari 28, amekutana na Mzee Eric Mchata na Kampuni
ya madini ya Uranium ya Mantra Tanzania kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo
baina ya pande hizo mbili.
Kikao
hicho, kinafuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Magufuli Januari 22 na Mzee Mchata wakati wa mkutano wa Kisekta
ulioshirikisha wachimbaji wadogo na wadau wa madini uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Wakati
akisikiliza kero za wachimbaji na wadau wa madini walioshiriki kikao hicho, Rais
Magufuli alipokea kero ya Mzee Mchata aliyemweleza kwamba amekuwa na mgogoro na
kampuni hiyo kwa kipindi cha takribani miaka 12 na bado hajapata suluhu.
Akijbu
kero iliyowasilishwa na Mzee Mchata, Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Madini
kuhakikisha mgogoro huo unafikia mwisho.
0 comments:
Post a Comment