Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alipokwenda kuutemebelea mti alioupanda tarehe 13.11.2017 wiki mbili baada ya kukabidhiwa ofisi na Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa huo Zelote Steven ambapo mti huo ameupanda katika kijiji cha mtowisa kilichofanyikia sherehe za siku ya kupanda miti kimkoa tarehe 19.1.2019.
Mkuu wa
mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewashauri wananchi wote wanaoharibu misitu
kwa kuchoma moto kwaajili ya kuwinda panya waanze kufuga kuku ili kuweza kuokoa
mazingira huku akiwataka
wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha wanamuandalia mipango
mikakati ya halmashauri zao katika upandaji wa miti ikiwa ni kufuata agizo la
serikali la kuitaka kila halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka.
Alisema kuwa moja
ya matokeo ya shughuli hizi za kibinadamu ni uharibifu mkubwa wa mistu na
vyanzo vya maji unaoweza kusababisha madhara makubwa kama kukosa mvua kwa
wakati, uzalishaji mdogo wa chakula na hata maradhi mbalimbali yanayotokana na
uharibifu wa mazingira na kuongeza kuwa ufanisi wa zoezi hili la upandaji miti unatia shaka
kutokana na kutosimamiwa vizuri na Viongozi wa Halmashauri zetu zote.
“Kwa hiyo naagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri
zetu kuwasilisha mpango mkakati wa upandaji miti kwa kipindi cha Mwaka huu,
ikiwa ni pamoja na kubainisha idadi ya miti waliyonayo na mahali ilipo pamoja
na ya Wadau wao wa utunzaji wa Mazingira, na maeneo ya kupanda. Mpango
huu unifikie ndani ya siku tano kuanzia leo,” Alisisitiza.
Vile vile alizitaka Taasisi za
Serikali kama shule, magereza na vyuo vya elimu kuanza kutumia nishati mbadala
ikiwemo ya “biogas” katika shughuli zao za mapishi ya chakula na kupunguza kasi
ya matumizi ya kuni kwani mkoa una mitambo 2 ya “biogas” katika Manispaa ya
Sumbawanga katika Vijiji vya Mtimbwa na Ntendo ambayo inatumika kama darasa la
kujifunzia ujuzi wa kutengeneza biogas kutokana na mabaki ya mifugo yetu.
Wakati akisoma taarifa ya halmashauri
juu ya zoezi la upandaji miti, Afisa Ardhi na malisili wa halmashauri ya Wilaya
ya Sumbawanga Juma Chande alieleza kuwa katika msimu wa mwaka 2018/2019 katika
kata 8 kati ya kata 27, halmashauri imeshapanda miti 292,899 ambayo ni asilimia
17.4 ya lengo na ufafanua kuwa halmashauri inaendelea kutoa elimu ya kutunza
mazingira, kupanda miti na kilimo mseto huku akitaja changamoto zinazorudisha
nyuma juhudi hizo.
“Miongoni mwa changamoto ni muitikio
mdogo wa wananchi katika utunzaji wa mazingira pamoja na hamasa nyingi kutolewa
kwao, mila na tamaduni za wananchi za uwindaji wa panya mathalani kusababisha
uchomaji wa miti wakati wa kiangazi mfano maeneo ya vijiji vya Msandamuungano,
Sandulula na Mpwapwa hivyo kuathiri misitu iliyopandwa.” Alimalizia.
0 comments:
Post a Comment