Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia watumishi
katika maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi kwenye viwanja vya
Nyerere Square jijini Dodoma, Januari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia watumishi katika maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma, Januari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano wa
wafanyakazi maarufu kama (solidarity forever) kwenye maandamano ya amani
ya vyama vya wafanyakazi, yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square
jijini Dodoma, Januari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watumishi wa Ofisi ya Bunge, wakipita mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, katika maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi,
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma, Januari 7, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) limeyataka makundi ya
wanasiasa kutowatumia wao kama njia ya kujitafutia umaarufu kwa kuzungumzia
masuala yao na badala yake wawaachie viongozi wa vyama hivyo kwa sababu
wanajitosheleza.
Pia shirikisho hilo limesema litaendelea kuiunga mkono na kushirikiana
na Serikali ya awamu ya tano pamoja na rais wake Dkt. John Magufuli na kwamba
watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya ajira zao.
Hayo yamesemwa leo (Jumatatu, Januari 7, 2019) na Katibu Mkuu wa TUCTA,
Yahya Msigwa katika hotuba yake aliyoitoa kwa wafanyakazi baada ya Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa kupokea maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi.
Watumishi wa taasisi mbalimbali leo wameandamana jijini Dodoma katika
viwanja vya Nyerere Squarekwa lengo la kumpongeza Rais Dkt. Magufuli kwa uamuzi
wake kufuta kikotoo kipya cha mafao ya wafanyakazi kilichopendekezwa katika
kanuni za sheria ya Mifuko ya jamii.
Katibu huyo wa TUCTA amesema mara nyingine makundi ya wanasiasa yamekuwa
yakisema maneno ambayo wao hawajayasema jambo ambalo limekuwa likiwachonganisha
na wadau wao wakiwemo wanachama pamoja na Serikali.
”Wafanyakazi wanaona fahari kwa sababu Rais Dkt. Magufuli anasikiliza
kero mbalimbali zinazowakabili na kuzitatua kwa wakati. Aliposema atafufua
Shirika la Ndege Tanzanzia amelifufua na sasa tuna ndege saba pamoja na ujenzi
wa miradi mkubwa ya umeme, barabara ambayo yote inaenda kutengeneza ajira.”
Hata hivyo, ameiomba Serikali ifanye uchunguzi kwenye miradi
inayotekelezwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa sababu hawana uhakika kama
miradi hiyo imerejesha fedha. Pia ameiomba Serikali iongeze mishahara kwa
watumishi wa umma.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema Serikali
ipo tayari wakati wote kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wafanyakazi ikiwa ni
pamoja na kuboresha mishahara na maslahi yao. “Wito wa Serikali ni kuwa
wafanyakazi watekeleze majukumu yao kwa uadilifu,weledi na kujituma ikiwa ndio
chachu ya kufikia malengo na ustawi wa nchi yetu.”
Kuhusu
suala la kupandisha mishahara, madaraja na maslahi ya wafanyakazi
kwa ujumla, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli alishalitolea
maelekezo na kwamba Serikali inayafanyia kazi maelekezo yake, hivyo amewaomba
wafanyakazi waendelee kuwa wavumilivu.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kulipa stahili za watumishi wa umma kwa
wakati na kulipa madeni hatua kwa hatua, ambapo kati ya Julai 2018
hadi Septemba 2018, Serikali imelipa sh. bilioni 184.9 za madai mbalimbali ya
watumishi.
“Kati
ya kiasi hicho Serikali imelipa shilingi bilioni 49 kwa ajili ya malimbikizo ya
mishahara kwa watumishi 28,214 ambayo yanajumuisha shilingi bilioni 19.2
walizolipwa walimu 16,214. Hata hivyo Serikali inaendelea na utafiti wa
tathmini ya kazi katika wizara na taasisi mbalimbali ili kupanga vizuri
mishahara na motisha kwa watumishi wa umma.”
0 comments:
Post a Comment