METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, January 15, 2019

SERIKALI YAFUTA MASHAMBA SITA YA MOHAMED ENTERPRISES

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimsikiliza Meneja wa Mashamba ya Mkonge ya Mohamed Enterprises ya Mazinde Korogwe mkoa wa Tanga Alhaji Imam Sheketo wakati alipofanya ziara katika mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019, kulia kwa waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akiwasikiliza wananchi wa Mabogo Korogwe mkoa wa Tanga wakati alipotembelea mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019.
Meneja wa Shamba la Mkonge la Mohamed Enterprises lilipo Korogwe mkoani Tanga Alhaj Imam Sheketo akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela sehemu ya mashine za kutengeneza katani katika shamba lilipo eneo la Mabogo Korogwe Tanga.

Na Munir Shemweta, KOROGWE
Serikali imeyafuta mashamba sita yenye ukubwa wa hekari 12,915.126 ya kampuni ya Mohamed Enterprises yaliyopo korogwe mkoa wa Tanga.
Uamuzi wa kufuta mashamba hayo unafuatia mapendekezo yaliyotolewa na halmashuri ya wilaya ya Korogwe kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu na baadaye maombi hayo kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wizara kwa nia ya kufutwa. 
Mashamba yaliyofutwa ni yale yaliopo eneo la Mombo, Mabogo pamoja na Kwalukonge wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Akizungumza mara baada ya kutembelea   mashamba hayo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.  Angeline Mabula alisema mashamba yaliyobatilishwa ni kati ya mashamba 14 yanayomilikiwa na kampuni ya Mohamed Enterprises Mazinde wilayani Korogwe  na kubainisha kuwa uamuzi huo unalenga  kujenga nidhamu kwa waliopewa rasilimali za serikali kuzingatia masharti ya uwekezaji.
Alisema, mara baada ya halmashauri ya wilaya ya Korogwe kupeleka mapendekezo ya kufutwa mashamba ya Mohamed Enterprises, wizara ya ardhi ilifanya ufuatiliaji juu ya mambo ya halmashauri husika la  kutoendelezwa mashamba na baada ya kujiridhisha ikawasilisha maombi hayo  kwa  rais na kuridhiwa.
Alisema, uamuzi huo wa Rais kuridhia ubatilishaji mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na Mohamed Enterprises unalenga kuhakikisha wote waliopewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wanazingatia masharti na taratibu za uwekezaji. 
Hata hivyo, Dk Mabula alisema mashamba ambayo hayajabatilishwa  yamewekewa utaratibu kwa nia ya kuyaboresha kwa kuwa baadhi yake yanahitaji maboresho kwa nia ya kufanya vizuri.
Ameitaka halmashauri ya Korogwe kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika eneo la mashamba yaliyofutwa na kipaumbele kwa watakaopewa maeneo katika mashamba hayo ni wananchi waliokuwa wakiishi katika mashamba hayo na sehemu itakayobaki atafutwe mwekezaji mwingine kwa kuwa lengo la serikali ni kuwa na uwekezaji wa viwanda.
Aidha, Dk Mabula alimpongeza Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela kwa kufanya kazi nzuri ya kufutilia na kusimamia maagizo mbalimbali tangu Rais John Pombe Magufuli alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa wa Tanga.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela aliwataka wananchi wa Korogwe kutovamia maeneo ya mashamba yaliyobatilishwa hadi hapo Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi katika mashamba hayo.
Alisema, ndani ya wiki hii ataitisha mkutano na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa huo pamoja na wale wa bodi ya Mkonge kuangalia matumizi ya ardhi iliyobatilishwa kwa wananchi na uwekezaji.
CAPTION PICHA                                                                                                                          
PIX NO 1-Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimsikiliza Meneja wa Mashamba ya Mkonge ya Mohamed Enterprises ya Mazinde Korogwe mkoa wa Tanga Alhaji Imam Sheketo wakati alipofanya ziara katika mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019, kulia kwa waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela.
PIX NO 2- Mkazi wa Mabogo Korogwe mkoani Tanga Said Mbazi Idawa akiwasilisha malalamiko yake wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula katika Mashamba ya Mkonge Korogwe mkoa wa Tanga.
PIX NO 3- Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akiwasikiliza wananchi wa Mabogo Korogwe mkoa wa Tanga wakati alipotembelea mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019.
PIX NO 4- Meneja wa Shamba la Mkonge la Mohamed Enterprises lilipo Korogwe mkoani Tanga Alhaj Imam Sheketo akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela sehemu ya mashine za kutengeneza katani katika shamba lilipo eneo la Mabogo Korogwe Tanga.
PIX NO 5- Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa wakimuongoza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula kuangalia eneo la mashine za kutengeneza katani katika shamba la Mohamed Enterprises lililopo Mabogo Korogwe mkoani Tanga. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA-WIZARA YA ARDHI)
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com