Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimsikiliza Meneja wa Mashamba ya Mkonge ya Mohamed Enterprises ya Mazinde Korogwe mkoa wa Tanga Alhaji Imam Sheketo wakati alipofanya ziara katika mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019, kulia kwa waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dk Angeline Mabula akiwasikiliza wananchi wa Mabogo Korogwe mkoa wa
Tanga wakati alipotembelea mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14
Januari 2019.
Meneja wa Shamba la Mkonge la Mohamed
Enterprises lilipo Korogwe mkoani Tanga Alhaj Imam Sheketo akimuonesha Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula pamoja na Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela sehemu ya mashine za kutengeneza katani katika
shamba lilipo eneo la Mabogo Korogwe Tanga.
Na Munir
Shemweta, KOROGWE
Serikali
imeyafuta mashamba sita yenye ukubwa wa hekari 12,915.126 ya kampuni ya Mohamed Enterprises yaliyopo
korogwe mkoa wa Tanga.
Uamuzi
wa kufuta mashamba hayo unafuatia mapendekezo yaliyotolewa na halmashuri ya
wilaya ya Korogwe kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa kwa muda
mrefu na baadaye maombi hayo kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na wizara kwa nia ya kufutwa.
Mashamba
yaliyofutwa ni yale yaliopo eneo la Mombo, Mabogo pamoja na Kwalukonge
wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea mashamba hayo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula alisema mashamba
yaliyobatilishwa ni kati ya mashamba 14 yanayomilikiwa na kampuni ya Mohamed
Enterprises Mazinde wilayani Korogwe na kubainisha kuwa uamuzi huo
unalenga kujenga nidhamu kwa waliopewa rasilimali za serikali kuzingatia
masharti ya uwekezaji.
Alisema,
mara baada ya halmashauri ya wilaya ya Korogwe kupeleka mapendekezo ya kufutwa
mashamba ya Mohamed Enterprises, wizara ya ardhi ilifanya ufuatiliaji juu
ya mambo ya halmashauri husika la kutoendelezwa mashamba na baada ya
kujiridhisha ikawasilisha maombi hayo kwa rais na kuridhiwa.
Alisema, uamuzi
huo wa Rais kuridhia ubatilishaji mashamba sita kati ya 14 yanayomilikiwa na
Mohamed Enterprises unalenga kuhakikisha wote waliopewa maeneo kwa ajili ya
uwekezaji wanazingatia masharti na taratibu za uwekezaji.
Hata
hivyo, Dk Mabula alisema mashamba ambayo hayajabatilishwa yamewekewa
utaratibu kwa nia ya kuyaboresha kwa kuwa baadhi yake yanahitaji maboresho kwa
nia ya kufanya vizuri.
Ameitaka
halmashauri ya Korogwe kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika eneo la
mashamba yaliyofutwa na kipaumbele kwa watakaopewa maeneo katika mashamba hayo
ni wananchi waliokuwa wakiishi katika mashamba hayo na sehemu itakayobaki
atafutwe mwekezaji mwingine kwa kuwa lengo la serikali ni kuwa na uwekezaji wa
viwanda.
Aidha, Dk
Mabula alimpongeza Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela kwa kufanya kazi nzuri
ya kufutilia na kusimamia maagizo mbalimbali tangu Rais John Pombe Magufuli
alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa wa Tanga.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela aliwataka wananchi wa Korogwe
kutovamia maeneo ya mashamba yaliyobatilishwa hadi hapo Halmashauri ya Wilaya
ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi katika mashamba hayo.
Alisema, ndani
ya wiki hii ataitisha mkutano na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa huo
pamoja na wale wa bodi ya Mkonge kuangalia matumizi ya ardhi iliyobatilishwa
kwa wananchi na uwekezaji.
CAPTION
PICHA
PIX
NO 1-Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula
akimsikiliza Meneja wa Mashamba ya Mkonge ya Mohamed Enterprises ya Mazinde
Korogwe mkoa wa Tanga Alhaji Imam Sheketo wakati alipofanya ziara katika
mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019, kulia kwa waziri ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela.
PIX
NO 2- Mkazi wa Mabogo Korogwe mkoani Tanga Said Mbazi Idawa akiwasilisha
malalamiko yake wakati wa ziara ya Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dk Angeline Mabula katika Mashamba ya Mkonge Korogwe mkoa wa Tanga.
PIX
NO 3- Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula
akiwasikiliza wananchi wa Mabogo Korogwe mkoa wa Tanga wakati alipotembelea
mashamba ya mkonge mkoani Tanga leo tarehe 14 Januari 2019.
PIX
NO 4- Meneja wa Shamba la Mkonge la Mohamed Enterprises lilipo Korogwe mkoani
Tanga Alhaj Imam Sheketo akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Dk Angeline Mabula pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela
sehemu ya mashine za kutengeneza katani katika shamba lilipo eneo la Mabogo
Korogwe Tanga.
PIX
NO 5- Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa
Gwakisa wakimuongoza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk
Angeline Mabula kuangalia eneo la mashine za kutengeneza katani katika shamba
la Mohamed Enterprises lililopo Mabogo Korogwe mkoani Tanga. (PICHA
ZOTE NA MUNIR SHEMWETA-WIZARA YA ARDHI)
No comments:
Post a Comment