Kufuatia
kukaidi Wito wa kuonana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa
Richard Kasesela kutokana na kufanya ununuzi haramu wa madini
ya dhahabu ikiwemo kufadhili uchimbaji haramu, Naibu Waziri Nyongo amevitaka
vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Iringa
kuwakamata Mansoor Almasi na Jacob
Mwapinga iwapo watashindwa kuripoti wenyewe katika Mamlaka zinazohusika.
Naibu
Waziri Nyongo ametoa agizo la kukamatwa wahusika hao baada ya kukiuka agizo la
kuonana na viongozi hao kwa hiari ambapo
walielekezwa kuonana na Naibu Waziri na Mkuu wa Mkoa Januari 15.
Pia,
kabla ya wito wa Naibu Waziri, awali, wahusika hao walitakiwa kuonana na Mkuu
wa Wilaya ya Iringa wakiwemo Maafisa Madini kwa ajili ya kuupatia suluhisho
mgogoro huo katika mgodi wa dhahabu wa Ulata, kijiji cha Ulata wilaya ya Iringa
unaomilikiwa na Ibrahimu Msigwa.
Naibu
Waziri Nyongo alibaini kuwa Mansoor na Mwapinga wanafanya ununuzi wa madini kinyume cha Sheria ikiwemo kufadhili shughuli za uchimbaji katika mgodi ambao siyo
wamiliki wake.
Pia,
Naibu Waziri ameelekeza baada ya
wahusika hao kukamatwa wanatakiwa kutoa maelezo kueleza ni lini watalipa kodi wanazodaiwa na
serikali baada ya kufanya shughuli hizo
bila kulipa kodi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wachimbaji hao,
Naibu Waziri Nyongo aliwaeleza kuwa, Serikali inamtambua Ibrahimu Msigwa kama
mmiliki halali baada ya kuwa na vibali vya kumiliki leseni ya mgodi huo na
hivyo kutoa wito wa kuonana na pande zote ili kuhakikisha kuwa anatoa suluhisho la mgogoro uliopo baina
ya Msigwa, Mansoor, Mwapinga na wachimbaji.
Akihitimisha
ziara yake mkoani Iringa Januari 15, Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa, amebaini
ukwepaji mkubwa wa kodi katika migodi ya
Ulata na Nyakavangala.
Amesema
wamiliki wa leseni wanaotumia mrabaha kwa ajili ya kufanya masuala mengine ya
kijamii wanakiuka taratibu na kueleza kuwa, fedha za kufanyia shughuli za
maendeleo zinapaswa kutoka katika fedha za Uwajibikaji kwa jamii ambazo
halmashauri zinapanga kupitia Baraza la Madiwani.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema wahisika Mwapinga na Almasi wana kiburi na kwamba
waliitwa kwa ajili ya kuongea ili ku[ata fursa ya kujieleza na a kueleza ni lini
watalipa mrabaha lakini wamekaidi hivyo
kinachofuatia ni wahusika kukamatwa.
Naibu
Waziri Nyongo alifanya ziaea katka mgodi wa Ulata Janauri 14 akilenga kukagua
shughuli za uchimbaji madini katika mgodi huo ikiwemo kutatua mgogoro uliokuwep
katika mgodi huo baina ya mmiliki halali Ibrahimu Msingwa, wanunuzi haramu
wa madini hayo Mansoor Almasi na Jacob Mwapinga.
Xxxxxxx xxxxxxxx
0 comments:
Post a Comment