Akizungumzia Msingi wa ziara hiyo Mhe Mgumba amesema kuwa ni Kukagua Miradi ya Maendeleo inatotekelezwa na serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe Raisi Dkt Jonh Joseph Pombe Magufuli katika jimbo hilo Pamoja na kuhamasiha wananchi Kujitolea katika ujenzi wa miundombinu ya Vyumba vya Madarasa kufuatia ufaulu Mkubwa wa watoto wanaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwezi huu wa kwanza.
Pia ziara hiyo itakuwa na msingi wa kusikiliza Kero na Changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo anaowawakilisha ili kwa kushirikiana nao Pamoja na Serikali yao kuzipatia ufumbuzi na kuzitatua.
Alisema kuwa Mafanikio hayo ya ufaulu mzuri wa wanafunzi umeleta changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 17 katika kata Saba kwenye tarafa za Mkuyuni na Ngerengere. shule hizo Mkuyuni Vyumba 7, Kinole 2, Kiroka 2, na Tomondo 3 kwenye tarafa ya Mkuyuni na Ngerengere Vyumba 3, Kidugalo 2 na Tununguo 1.
Pia katika ziara hiyo Mhe Mgumba amepata fursa ya Kutembelea Kituo cha Afya Mkuyuni kujionea hali ya ujenzi unavyoendelea.
Pichani Mhe Mgumba akiwa na Mhr Diwani wa kata hiyo Mhe Mwinyi Buyi na viongozi wengine wakikagua hali ya ujenzi huo.
0 comments:
Post a Comment