METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, January 28, 2019

Mdau wa Utali Tanzania Nangasu Warema atoa atoa ya moyoni kuhusu sekta ya utalii nchini



Amesema zipo sababu 3 muhimu zinazofanya sekta ya utalii nchini isikue kwa kasi.

Aidha mdau huyo ameleeza kuwa kama changamoto hizo zingeweza kukua sekta hii ingekuwa kwa kasi kuliko hata nchi za wenzetu za jirani.

Bi Nangasu Warema Amesema sekta ya  utalii ni moja kati ya sekta zinasaidia kukua kwa pato la taifa nchini.

Warema amefafanua kwamba Tanzania ni nchi ya pili yenye vivutio vingi vya utalii duniani lakini ongezeko la watalii nchini linakuwa kwa taratibu sana.

Zipo Changamoto kuu tatu ambazo kama serikali itakuwa na dhamira ya maksudi kushirikiana na wadau wa sekta ya utalii na kuzitatua kutakuwa na ongezeko kubwa la watalii Tanzania.

Mdau huyo wa Utalii nchini ambae kampuni yake ndio ilioingiza vivutio vyetu vya utalii chini mlima Kilimanjaro na Ngorongoro kuingia kwenye maajabu saba ya Dunia na kuvitangaza dunia nzima hatimae kuiletea Tanzania ushindi ameeleza kuwa kama atapata nafasi ya kuzungumza na Rais Magufuli atamueleza sababu hizi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com