METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 6, 2020

Wananchi waliojenga karibu na Miundombinu ya Reli Mkoa wa Arusha Watakiwa kuondoka

Na Agnes Geofrey

Naibu waziri wa ujenzi ,uchukuzi na mawasiliano Mh Atashanta Nditiye amewataka wananchi kuachia maeneo yao yaliyo karibu na reli kwa kutii Sheria Kama inavyosema pawepo na mita 30 kila upande zisizo fanyiwa chochote huku kutoendelea na shughuli zozote za kibinadamu.

Ameyasema hayo wakati akifanya ziara ya ukaguzi wa reli ambayo ilianzishwa mnamo 1905ya kuanza safari za Arusha -Moshi ,Moshi -Arusha kwani reli inaanza kufanya kazi wiki mbili zijazo hivyo Ni vyema wananchi wakalindana wao kwa wao ili kuweza kuitunza  reli hiyo kwani Ni ya kwao wanatakiwa wailinde na sio kuweka vyuma ili kusababisha ajali kwani baadhi ya madhara hayo husababishwa na shughuli zao wanazozifanya karibu na reli hiyo.

Aidha Mhe Waziri ameongeza kuwa zaidi ya miaka 30 reli hiyo ilikuwa haitumiki Ila alifanikiwa kusafiri kwa Mara ya kwanza kwa lengo la kujilidhisha Kama reli iyo inafaa huku akiwashukuru Shirika la reli Tanzania (TRC) kwa kazi yao nzuri wayoifanya,kwani treni hiyo Ni ya Watanzania wote na kutoa wito kwa viongozi wa wilaya wote nchini ambao reli inapita karibu na wilaya zao wafanye vikao na viongozi wa vijiji,tarafa na wilaya yote ili kuwaelewesha wananchi umuhimu wa reli hiyo kwani treni haimgongi mtu Bali mtu ndio anaigonga treni.

Nae Kaimu Mkurugenzi mamlaka ya udhibiti usafiri nchi kavu (LATRA)injini  Lameck Kamando, amesema kuwa Mambo yote ambayo Mh waziri ameyatolea maelekezo wataenda kuyasimamia ipasavyo ili  kulinda na kutunza rasilimali hiyo na kutoa elimu kwenye shule ambazo zipo karibu na reli ili kuwa na taadhali juu ya matumizi ya reli na kuitumia vizuri kwa matumizi ya Sasa na vizazi vijavyo.

Aidha nao baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Arusha bi Theresia Mshanga na Alpha Ibrahimu Wamesema kuwa wanamshukuru Mh Rais  kwa kuwarudishia usafiri huo kwani watu wa kipato Cha chini walikuwa wakipata tabu hivyo Kupitia treni hiyo itapelekea kupata ajira huku wakiomba kutolewa kwa taarifa mapema katika eneo la daraja mbili kwani reli hiyo ipo karibu na kituo Cha magari huku wafanyabiashara wakiendelea na shughuli zao.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com