METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 31, 2018

TWENDE NA HII 2019

Na Debora Charles Kiyuga✍🏽

Jifunze KUJIAMINI sana kabla hujataka mtu mwingine akuamini kwa sababu ni rahisi kuanguka au kuchukua mitazamo ya watu wengine kama hujajiamini wewe KWANZA.

Jifunze KUJITAMBUA sana kabla hujataka mtu mwingine akutambue kwa sababu ni rahisi kukosa Uelekeo na kubebwa na maneno ya watu wengine kama hujajitambua wewe KWANZA.

Jifunze KUJISIMAMIA sana kabla hujataka mtu mwingine akusimamie kwa sababu ni rahisi kuyumbishwa na kuangushwa na watu wengine kama hujasimama wewe KWANZA.

Jifunze kuijua NDOTO yako sana kabla hujataka mtu mwingine aijue kwa sababu ni rahisi kukatishwa na kupotezwa na watu wengine kama hujaijua wewe KWANZA.

Jipe changamoto ya KUTHUBUTU katika kila jambo lenye mafanikio linalokupa HOFU. Itafute nguvu yako mwenyewe. Waza, Panga, Thubutu, Tekeleza kwa bidii na uwezo wako wote.

JARIBU vitu vingi kadri uwezavyo ili vikupe uwezo wa kujipambanua na kujua ni wapi hasa unastahili kuwa.

Tafuta UHAKIKA wa maisha unayoamini kuwa ndiyo MAFANIKIO yako. Miliki Furaha yako, miliki AMANI yako, miliki Mahusiano yako pamoja na Upendo wako kwa watu wengine.

Daima mtegemee MUNGU na kubali kuongozwa na watu sahihi katika maisha yako. Ongeza BIDII katika Ibada pamoja na Kazi na kwa namna yeyote ile, Ishi UHALISIA wa maisha yako.

NAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2019.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com