Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wakati alipowasili katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Desemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wakati alipowasili katika kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwa, Desemba 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema jumla ya shilingi bilioni 222
zimelipwa na Serikali kwa wakulima wa zao la korosho na kuwataka wakulima wawe
na subira.
Amesema wakulima walioanza kulipwa ni wale wenye kilo zisizozidi kilo
1,500 na wale wenye kilo zaidi ya 1,500 na kuendelea Serikali inaendelea na
uhakiki kisha watalipwa.
”Fedha zipo, hakuna mkulima ambaye atapoteza haki yake wote watalipwa.
Tunaendelea na uhakiki kwa wale wenye korosho nyingi ili kubaini kama
hawajanunua kangomba.”
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Desemba 30, 2018)
alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Nandagala ‘A’ baada ya kufungua ofisi
ya CCM kata ya Nandagala.
Amesema baadhi ya watu wamekutwa na kilo zaidi ya 1,500 na wameshindwa
kuonesha mashamba yao ya mikorosho, hali inayodhihirisha kwamba amenunua
kupitia kangomba.
Waziri Mkuu amesema baadhi ya waliokutwa na korosho nyingi ni vijana
wadogo ambao hawana hata uwezo kifedha hivyo Serikali itahakikisha inawakamata
watu wanaowatuma.
Amesema lengo la Serikali inayoongizwa na Rais Dkt. John Magufuli ni
kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao, hivyo biashara ya kangomba
lazima lidhibitiwe.
Waziri Mkuu ambaye leo ameanza ziara yake kwa kikazi wilayani Ruangwa,
Mkoani Lindi amesema zoezi la ulipaji kwa wakulima wa korosho linaendelea,
wakulima wawe na subira.
Serikali iliamua kununua korosho zote za mwaka huu baada ya kubaini
wafanyabiashara wamepanga kuwadhulumu wakulima kwa kupanga kununua kwa bei
ndogo.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametembelea eneo la ujenzi wa shule ya sekondari ya kata
ya Matambalale wilayani Ruangwa ambapo amewataka wahakikishe ujenzi
unakamilika.
Amewataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na kuhakikisha wanachangia
nguvu kazi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ili mwakani wanafunzi waanze
kusoma.
”Tunataka tuondoe dhiki ya watoto wetu kutembea umbali mrefu hadi
Namichiga kutafuta elimu, tunataka watoto wetu wote wasome katika maeneo yaliyo
karibu na makazi yao.”
Amesema wanafunzi zaidi ya 200 wamefaulu na hawana pa kwenda hivyo ni
lazima ujenzi wa shule zote za sekondari za Matambalale, Chibura na Ruchelegwa
ukamilike.
Waziri Mkuu amesema hadi Januari 10, 2019 shule hizo zote lazima ujenzi
wake ukamilike ili wanafunzi waanze kusoma, hivyo viongozi washirikiane na
wananchi kukamilisha ujenzi.
0 comments:
Post a Comment