Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mti wa Korosho zinazozalishwa kwa ajili ya mbegu katika Kituo cha Utafiti wa kilimo TARI-Naliendele Mkoani Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi tarehe 1 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mche wa Korosho unaozalishwa katika Kituo cha Utafiti wa kilimo TARI-Naliendele Mkoani Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi tarehe 1 Disemba 2018, Wengine pichani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti TARI-Naliendele Dkt Fortunatus Kapinga (Kulia).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua akikagua shamba darasa kwa ajili ya korosho katika Kituo cha Utafiti wa kilimo TARI-Naliendele Mkoani Mtwara wakati akiwa katika ziara ya kikazi tarehe 1 Disemba 2018.
Miche ya korosho katika Kituo cha Utafiti wa kilimo TARI-Naliendele Mkoani Mtwara ikiwa katika kitalu nyumba (Green House) kabla ya kupelekwa kwa wakulima.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Uongozi
wa Kituo cha Utafiti wa kilimo cha TARI-Naliendele na Chuo cha Kilimo
Naliendele umepewa miezi saba kuanzia Disemba mosi mwaka huu 2018 mpaka mwezi
Juni 2019 kuweka alama ya mipaka ya kudumu (Beckon) kwenye maeneo yao yote.
Agizo
hilo limetolewa tarehe 1 Disemba 2018 na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)
wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi akiwa katika ziara ya kikazi katika
Kituo na Chuo hicho Mkoani Mtwara.
Mhe
Hasunga amepiga marufuku kwa wananchi kuingia katika maeneo hayo kwa kufanya
shughuli yoyote kwani eneo hilo ni maalumu na limetengwa kwa ajili ya chuo na
kituo hicho cha utafiti.
Alisema
kuwa Kituo cha utafiti TARI-Naliendele kinaongoza kwa utafiti wa mbegu za mazao
mbalimbali ikiwa ni pamoja na korosho ambayo inatoa mchango mkubwa Duniani hivyo
ni lazima kujikita katika kuandika miradi mbalimbali ya kutafuta fedha katika
Taasisi za ndani na nje ya nchi.
“Mkipata
miradi na fedha za kutosha utafiti wenu utaimarika na kurahisisha huduma za
utekelezaji wa majukumu yenu ikiwa ni pamoja na kuimarisha utafiti” Alisisitiza
Vilevile
amewataka kusimamia vizuri miradi iliyopo kwa kuongeza uzalishaji na tija ili
kuingiza kipato kitakacho rahisisha utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kuimarisha
Taasisi na Chuo hicho kujitegemea.
Katika
hatua nyingine Waziri Hasunga ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI-Naliendele
kuongeza kasi ya utafiti ili kuyakabili magonjwa mbalimbali ya mazao
yanayojitokeza mashambani kwa wakulima nchini.
Akijibu
risala za chuo na Taasisi hiyo kuhusu upungufu wa watumishi, Waziri Hasunga
alisema kuwa katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili serikali ilikuwa inafanya
uhakiki wa watumishi hewa na wenye vyeti feki hivyo upungufu ulisababishwa na
kubainika kwa watumishi hao walioondolewa kazini.
Hata
hivyo baada ya kukamilika kwa zoezi hilo serikali ilitoa ruhusa ya kupanishwa madaraja
kwa watumishi wote ambao walikuwa hawajapandishwa madaraja.
Aidha,
Mhe Hasunga amewataka wafanyakazi wote wa Chuo cha Itafiti wa Kilimo na Kituo
cha Utafiti TARI-Naliendele kufanya kazi kwa umoja na mshikamano huku
akisisitiza zaidi kuhusu uwajibikaji, nidhamu na weledi.
0 comments:
Post a Comment