Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Kushoto ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) wakati wa Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018.
Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof Joseph Buchweshaija na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakifatilia Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo- Mtwara
Serikali
imeagiza korosho zote inazonunua kwa wakulima kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao
mchanganyiko kuanza kubanguliwa nchini.
Agizo
hilo la serikali limetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo
tarehe 8 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda
vya kubangua korosho kwenye ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara.
Hasunga
alisema kuwa Mkakati wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Mhe Dkt
John Pombe Magufuli ni kuwanufaisha wakulima nchini hivyo maamuzi ya kununua
korosho ni sehemu ya maamuzi mema kwa manufaa ya wakulima wote.
Alisema
wakati serikali inaendelea kukamilisha uhakiki wa wakulima wa korosho pamoja na
kuendelea na malipo ya wakulima mpaka hivi sasa tayari wakulima 77,380
wamekwishalipwa hivyo hakuna korosho itakayoruhusiwa kusafirishwa kwenda nje ya
nchi bila utaratibu maalumu badala yake korosho zote zitabanguliwa nchini.
Mhe
Hasunga aliongeza kuwa Korosho zitakazoruhusiwa kwenda nje ya nchi ni zile Tani
2000 pekee zilizonunuliwa mnadani na kampuni mbili kwa utaratibu uliokuwa
ukitumika awali.
“Hakuna
kampuni yoyote wala mfanyabiashara yoyote anayeruhusiwa kusafirisha korosho nje
ya nchi baada ya tamko la serikali kutolewa” Alikaririwa Mhe Hasunga
Aliongeza
kuwa kutokana na uamuzi huo wa serikali imechukua takwimu zote za korosho zilizozalishwa
mwaka jana ambazo zilikuwa bado hazijabanguliwa hivyo haitegemei kusikia
wafanyabiashara wakisema wana korosho nyingi walizohifadhi badala yake kuwa
wazalendo kwa kusema ukweli.
“Tuwe
na uwezo wa kubangua ama hakuna lakini korosho zote zitabanguliwa nchini, hivyo
wito wangu kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya ubanguaji usiku na mchana”
Alisema
Mhe
Hasunga aliongeza kuwa serikali imeanza mchakato wa kuwafuatilia baadhi ya
wafanyabiashara wenye uwezo wa kujenga viwanda kwa kufunga mitambo ndani ya
muda mfupi.
Kwa
upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) amesema
kuwa serikali imedhamiria kuimarisha uchumi wa viwanda hivyo Serikali
haitakubali kuhujumiwa inapoendelea kuboresha uwekezaji, uanzishaji na
uendelezaji wa viwanda.
Alisema
kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na upendo hivyo wafanyabiashara kote Duniani
wana wajibu wa kujitokeza na kuanzisha biashara zao pasina kadhia yoyote.
Aliongeza
kuwa mawakala wanaotumiwa kuvuruga uchumi wa viwanda na serikali kwa ujumla
wake watachukuliwa hatua zinazopaswa kwa mujibu wa sheria.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment