Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho kutoka katika mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara leo tarehe 9 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Kushoto ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) wakikagua korosho zikiwa kwenye kifungashio tayari kwa kuingia sokoni wakati akizungumza wa mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara leo tarehe 9 Disemba 2018.
Mkutano ukiendelea
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho kutoka katika mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara leo tarehe 9 Disemba 2018.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo- Mtwara
Hadi
kufikia jana tarehe 8 Disemba 2018 serikali imefanikiwa kuwalipa jumla ya
wakulima 82,835 katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Jumla
ya fedha iliyolipwa kwa wakulima hao ambao tayari wamefanyiwa uhakiki ni Bilioni
83 ambapo katika mkoa wa Mtwara wakulima 50,835 wamelipwa mkoa wa Lindi
wakulima 22,131 na Mkoa wa Ruvuma ni wakulima 9,445
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 9 Disemba 2018
wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho kutoka katika
mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro uliofanyika katika ukumbi
wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara.
Aidha,
Mhe Hasunga alisema kuwa jumla ya vyama 328 vimefanyiwa uhakiki kati ya vyama
504 vilivyopo katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ambapo jumla ya vyama 319
vimekwishalipwa.
Vilevile
amewatoa hofu wananchi wanaopotoshwa kuwa bado wakulima hawajalipwa kiasi
chochote cha fedha huku akisisitiza kuwa wakulima wanalipwa kupitia njia ya
benki hivyo wanapaswa kuwa na utamaduni wa kwenda benki.
Mhe
Hasunga alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kuwanufaisha wakulima wa korosho
ambapo tayari amewaelekeza watendaji wa Bodi ya Korosho Tanzania kuwasajili
wakulima wote wa korosho ili watambulike.
Waziri
Hasunga alisema kuwa kikao hicho kina lengo la Kujadiliana na kukubaliana
utaratibu uliopangwa na serikali katika ubanguaji wa korosho mwaka 2018/2019
kwa kuelekeza ubanguaji kufanyika nchini ili kuwanufaisha wananchi katika ajira
hiyo.
“Tumeiona
changamoto ya mitaji kwa wabanguaji wadogo nchini sambamba na wabanguaji
wakubwa hivyo ili serikali iwarahisishie upatikanaji wa mitaji tumeamua kuwapa
kazi ninyi wenyewe” Alisisitiza
Aliongeza
kuwa swala la uhakiki limejikita zaidi kubaini udanganyifu unaofanywa na baadhi
ya wahujumu wa biashara ya korosho “Kuna watu walikuwa wametoa akaunti za benki
lakini zinatofautiana na majina ya watu waliwasilisha korosho zao kwenye
maghala ya kuhifadhia korosho” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa
“Tulipoona
soko la korosho linayumba huku lengo la serikali likiwa ni kutaka kuonana
wakulima wananufaika tuliamua kuingilia kati na kuanza kununua korosho zote na
kwa kwenda mbele Zaidi tumeamua kubangua korosho zote hapa hapa nchini”
MWISHO
0 comments:
Post a Comment