METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, November 29, 2018

WAZIRI WA KILIMO MHE HASUNGA AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI BODI YA KOROSHO MJINI MTWARA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 29 Novemba 2018 amekutana na kufanya kikao kazi na wafanyakazi wa Bodi ya Korosho kwenye ukumbi wa CBT Mjini Mtwara.

Katika kikao hicho Mhe Waziri amesisitiza umuhimu wa watumishi hao kufanya kazi kwa bidi, Juhudi, Uadilifu na Maarifa ili kuisaidia serikali kufikia malengo yake.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilikuwa na majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufahamiana na kujifunza majukumu ya Bodi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Ndg Dunstan Kaijage akiwasilisha taarifa ya Bodi hiyo wakati wa kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kwenye ukumbi wa CBT Mjini Mtwara, Tarehe 29 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com