METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, November 29, 2018

WANAHARAKATI SENGEREMA WABUNI MBINU MPYA YA KUINUSURU JAMII NA UKANDAMIZAJI HAKI ZA MTOTO WA KIKE


Mwezeshaji wa kitaifa na kimataifa ambaye pia ni Mratibu wa FAWE Tanzania Bi. Neema Kitundu akitoa somo kwa washiriki wa Semina ya vitendo na sanaa katika harakati ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto.
 Binti huyo huyo ndiye mteka maji, ndiye mfanya usafi, ndiye mpishi pishi na hata nyakati nyingine kuwatumiwa kwenye shughuli za biashara ndogondogo ambapo majukumu hayo hupitiliza kiasi cha kumnyima mwanya  wa kufuatilia masuala ya elimu.


Wazazi wengine wamekwenda mbali zaidi na kuwasitisha masomo mabinti zao ili kuwaoza wapate mali.



Ukosefu wa elimu, mila na desturi mbovu, kipato duni cha familia, tamaa za kimwili na wazazi kukwepa majukumu yao ni moja kati ya yale yanayo chochea kasi ya vitendo vya ukatili kwa mtoto wa kike kushamiri.



Midahalo mingi imefanyika, makongamano, mikutano na hata semina lakini bado hali ni tete.



Kwa kuliona hilo wanaharakati wilayani Sengerema mkoani Mwanza, wameamua kuja na mpango wa kuielimisha jamii kwa njia mbadala ya maigizo ambapo hapa waigizaji ni wakuu wa idara mbalimbali za Serikali na Taasisi za kiraia.



Watu maarufu na wanaotambulika kwenye nyadhifa mbalimbali katika jamii na ngazi mbalimbali serikalini kama vile wakuu wa wilaya, wakurugenzi, mabwana na mabibi afya, wachungaji na mashekhe, wazazi na watendaji wa vijiji na vitongoji ndiyo waigizaji na waelimishaji.



Ni katika mradi wa mwaka mzima uliochini ya FAWE Tanzania, ukiratibiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA)

"Kwa muonekano huu wa baba na mama, mnajifunza nini na kipi hakipo sawa" Mwezeshaji wa kitaifa na kimataifa ambaye pia ni Mratibu wa FAWE Tanzania Bi. Neema Kitundu akitoa somo la picha na sanaa kwa washiriki wa Semina ya vitendo na sanaa katika harakati ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto.
Mratibu wa wa mpango wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bi. Viola Muhangi Kuhaisa akizungumza na washiriki wa Semina ya vitendo na sanaa katika harakati ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto.


 Sehrmu ya washiriki.
 "Jibu ndiyo au siyo kwa maswali hayo"  Mwezeshaji wa kitaifa na kimataifa ambaye pia ni Mratibu wa FAWE Tanzania Bi. Neema Kitundu akitoa somo la picha na sanaa kwa washiriki wa Semina ya vitendo na sanaa katika harakati ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto.

 Haki ya kutobaguliwa

Ubaguzi wa mtoto umegawanyika katika makundi mbalimbali, katika yote yapo makundi makuu mawili. Ubaguzi wa kijinsia ambao mtoto wa kike au wa kiume anaweza kubaguliwa na wazazi, walezi au jamii. Upo ubaguzi unaotokana na hali yake ya kimaisha kama vile utajiri au umasikini, ulemavu, ugonjwa, uyatima na jinsi anavyoonekana mbele za watu. 
Mfano wa kuumiza ni ubaguzi wa kimfumo ambao nchini takwimu zinaonyesha asilimia moja tu ya watoto wenye ulemavu wanoandikishwa kujiunga na elimu ya msingi. Hii inaathiriwa na mtazamo wa kijamii dhidi ya watoto hawa kwani wazazi huwafungia kuficha aibu, hivyo kunyimwa fursa kupata elimu.
 Viongozi kada mbalimbali wako hapa.


Zile tunazodhani ni haki za watoto kumbe ni fursa za kulea kwetu wazazi. Uporomokaji wa maadili duniani umefanya mataifa kutiana vitanzi kuhakikisha watoto wanastawi kupitia mikataba na matamko ya Umoja wa Mataifa na kwingineko. Pamoja na kuwapo ‘haki’ hizi bado baadhi ya wazazi wanaodhani ni ‘Uzungu’ kumpatia mtoto mahitaji yake ili akue vizuri.


Haki ya kuendelezwa
Kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya Mtoto Tanzania, maendeleo ya mtoto yanahusiana na mtoto kuwa na kiwango kinachokidhi makuzi kimwili, kiakili, kiroho, kimaadili na kijamii. Ili mtoto aweze kukua vizuri anahitaji kutunzwa, kuongozwa na kulelewa katika misingi mizuri. Mathalani, kuendelezwa kwa mtoto kimwili ni kukua kimaumbile na uzito kwa uwiano wa umri. 
Hali hii inategemea lishe na huduma bora za afya ikiwamo kupatiwa chanjo zote muhimu na upatikanaji wa viinilishe vyote muhimu. Maendeleo ya mtoto yanahitaji jitihada kutoka kwa mzazi, jamii na Serikali
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com