Jeshi la
polisi nchini kwa kushirikiana na asasi za kiraia zinazotetea haki na maslahi
ya watoto na wanawake zimetakiwa kuhakikisha zinasambaza elimu katika kata zote, ikiwemo kufanya makongamano pamoja na kutoa matangazo kwa wingi
kwenye Tv na redio ili wananchi wajua madhara ya ukatili wa kijinsia kwa
wanawake na watoto.
Afisa wa Polisi kutoka Dawati la jinsia Mkoa wa kipolisi Kimara Afande Anna Mihayo akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wanaharakati wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS)
Hayo yameelezwa
mapema wiki hii jijini Dar es salaam na Afisa wa polisi kutoka Dawati la jinsia Mkoa
wa kipolisi Kimara Afande Anna Mihayo wakati akitoa elimu kwa wanaharakati wa
GDSS kuhusu nafasi ya mwananchi katika kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake
na watoto kupitia Dawati la Jinsia.
Afisa huyo
amesema kuwa ili kufanikisha jambo hili ni vema wananchi kushirikiana kwa
pamoja na jeshi la polisi kwa kuweza kuwafichua watekelezaji wa ukatili huo kwa
kuwa ni watu tunaoishi nao katika maisha yetu ya kila siku.
Aidha ameongeza
kuwa zipo mbinu mbalimbali ambazo wananchi wanaweza kuzitumia ili kuweza
kupunguza kama sio kulimaliza kabisa tatizo hili moja wapo ikiwa ni kutumia waandishi
wa habari ili kuweza kusambaza habari kwa jamii na vyombo husika vitasikia na
kuweza kuchukua hatua stahiki.
Wanaharakati wa semina za GDSS wakifuatilia semina kwa makini.
Aliendelea kusema
kuwa mpaka leo hii bado kuna baadhi ya wananchi wanaogopa kutoa taarifa polisi
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uoga wa kuongopa kituo au kuogopa kujenga
uhasama na majirani au ndugu.
“Wananchi wengi
wanakuwa na taarifa muhimu za watu wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia kwa kuwa
mara nyingi watekelezaji wa mambo haya wanakuwa ni ndugu wa karibu au majirani,
hivyo walio wengi uogopa kupewa ubaya na familia au jirani, basi watu
wananyamaza kimya mpaka tatizo linapokuwa kubwa kama muhanga kuuwawa au kujeruhiwa
vibaya ndipo wanakuwa tayari kuongea ukweli”. Alisema Afande Anna
Lakini pia
baadhi ya wanaharakati wamelalamikia swala la rushwa katika vituo vya polisi kwa
kusema kuwa baadhi ya polisi wakipewa fedha na muhusika wa utekelezaji wa
ukatili huo wanaamua kufuta kesi kwa madai kuwa muende mkayamalizie nyumbani
bila mtuhumiwa kuchukuliwa hatua yeyote.
Kwa upande
wake Mwanaharakati Nyanjura Kalindo alisema kuwa jambo hili bado ni gumu
kutokana unapeleka kesi polisi ya mtoto aliyebakwa na mlezi wake kesi ikifika
kule polisi Yule mlezi akifungwa na huyu
mtoto huku anakosa msaada na pia familia inachukua hatua ya kumtenga Yule mtoto
na kugoma kumpa mahitaji yake muhimu kwa kuwa amesababisha kufungwa kwa ndugu
yao.
Semina ikiendelea.
0 comments:
Post a Comment