Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akisikiliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Pamoja Mining Ltd na Mkazi wa Nyarugusu Salum Othman (hawapo pichani) katika Ofisi ya Halmashauri ya Bukombe. Kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa kwanza kulia mbele) akisikiliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Pamoja Mining ltd na Mkazi wa Nyarugusu Salum katika Ofisi ya Halmashauri ya Bukombe. Wengine katika picha ni Wafanyakazi kutoka Ofisi ya Madini Geita na kampuni ya Pamoja Mining Ltd.
Na
Rhoda James – Bukombe
Naibu
Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo nchini kuhakikisha
kuwa leseni za uchimbaji Madini zinazotolewa na Wizara kupitia Tume ya Madini ikiwemo
mikataba ya ubia wanayongia na Kampuni mbalimbali kutokuwa chanzo cha migogoro
nchini.
Naibu
Waziri Biteko aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akisuluhisha mgogoro
uliokuwepo kati ya Kampuni ya Pamoja Mining Ltd na Mkazi wa Nyarugusu Salum
Othman ambaye aliilalamikia kampuni hiyo kwa kukiuka mkataba waliojiwekea kati
yao.
Akizungumza
katika kikao hicho cha usuluhishi, Naibu Waziri Biteko alisema kuwa, wachimbaji
wadogo wanapoingia mikataba na kampuni yoyote ile yenye nia ya kuwa na ubia na Mzawa
ni lazima wazingatie na kukubaliana juu ya mikataba wanayoingia kwa kuwa, pindi taratibu zinapokiukwa zinaichafua nchi.
“Mikataba hii mnayoingia mjue ya kuwa nyinyi
mnakuwa ni taswira ya nchi sasa mkikiuka mnakuwa mnaichafua nchi yetu, lazima mzingatie
makubaliano mnayojiwekea nyie wote, mwekezaji na mzawa,” alisema Biteko.
Aidha,
aliainisha baadhi ya masuala ambayo yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kuingia
mikataba na wabia na kueleza kuwa ni pamoja
na kuangalia uhai wa leseni zao, kusajili mikataba yao kwenye Tume ya Madini,
kuhakikisha kuwa eneo au biashara wanayoingia haina migogoro, wazawa kujua kuwa
wanatakiwa kuwa na asilimia angalau zisizopungua 25 na kuhakikisha kuwa kodi
zote za serikali zinalipwa kwa wakati.
Vilevile,
Naibu Waziri Biteko alimtaka, Othman ambaye ni mlalamikaji kuhusu ukiukwaji wa
mkataba kati yake na Kampuni ya Pamoja Mining Ltd kuhakikisha kuwa wanazingatia
sheria zote ili pande zote mbili ziweze kufanya kazi kwa tija na bila kukwepa kodi za serikali.
Pia,
alitumia fursa hiyo kuzitaka Ofisi za Madini kote nchini kuhakikisha kuwa
zinaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo ili matatizo kama hayo
yanayojitokeza sasa yasiendele kujitokeza kwani ni wajibu wa Wizara kuhakikisha
kuwa migogoro baina ya wachimbaji na
wawekezaji inakwisha.
Naye,
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda alimshukuru Naibu Waziri
Biteko kwa kusuluhisha mgogoro huo ambao umedumu kwa kipindi kirefu nakueleza kuwa,
ofisi hiyo itaendelea kuzingatia na kutekeleza maagizo hayo kwa mujibu wa
sheria.
MWISHO,
0 comments:
Post a Comment