Na
Mwandishi Wetu, Mwanza
WACHORAJI
wa jengo jipya la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, wametakiwa
kuharakisha ili serikali itangaze zabuni ujenzi uanze haraka.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema jana mkoani
hapa alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kiwanja hicho
ambayo ipo kwenye maboresho makubwa.
Mhe.
Kamwelwe amesema kukamilika kwa michoro hiyo ya jengo la kisasa kutasaidia
serikali kupitia wasimamizi wa ujenzi huo Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS), kutangaza zabuni na kupatikana kwa mkandarasi atakayejenga jengo
hilo.
“Kiwanja
cha ndege kinashughuli nyingi na jengo la abiria ni kityu muhimu sana, hivyo
ninaharakisha hao wachoraji wajitahidi kufanya haraka ili kukamilisha michoro
hiyo,” amesisitiza Mhe. Waziri.
Hatahivyo,
amesema ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa jengo la mizigo ambalo lipo mita
chache kutoka eneo la abiria, ambapo ndege za mizigo zimejengewa maegesho yake
rasmi tofauti na awali zilikuwa zikishusha upande wa ndege za abiria.
Halikadhalika
ametembelea jengo la kisasa la kuongozea ndege, ambalo nalo limekamilika kwa
asilimia 90 na kuridhishwa na utendaji wa Mhandisi Mkazi, Godfrey Asulumenye wa
Kampuni ya Unetec ya Dubai, pamoja na eneo linapojengwa rada.
“Nimeridhika
kuna maendeleo kwa kiasi kikubwa tofauti na nilivyopita awali, sasa kuna
tofauti maboresho yamekamilika kwa asilimia kubwa na imebaki sehemu za
kumalizia tu, ninaimani kwa kiasi kikubwa mkandarasi huyu atakamilisha kwa
wakati na kuboresha zaidi sehemu ambazo wanaona hazijakaa sawa kabla ya
kukabidhi,” Mhe. Kamwelwe.
Mhandisi
Asulumenye amesema maboresho hayo yamehusisha ujenzi wa jengo la mizigo, jengo
la kuongozea ndege, Kituo cha umeme, urefushaji wa barabara ya kutua na kuruka
kwa ndege kwa mita 700 na ikikamilika itakuwa na urefu wa Km4.
Maboresho
mengine kwa mujibu wa Mhandisi ni pamoja na uwekaji wat aa za kuomgozea ndege
(AGL), mifereji mikubwa ya kupitisha maji ya mvua, maegesho ya ndege, mifumo ya
maji taka na matenki ya maji safi.
Kiwanja
cha Ndege cha Mwanza kwa sasa ni daraja la 4C kinauwezo wa kuhudumia ndege za
abiria 300 na maboresho yakikamilika kitapanda na kuwa daraja la 4D. Takwimu
zinaonesha kinahudumia abiria 500,000 kwa mwaka ila matarajio ni kufikia abiria
milioni mbili (2) baada ya maboresho kukamilika.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment