mwakilishi wa Mradi wa MHRP Bw. Riziki Kasimu
(kulia) akimkabidhi funguo za gari litakalotumika kuongeza nguvu za mapambano
dhidi ya maambukizi ya Ukimwi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
(kushoto) mbele ya wadau dhidi ya maambuzi hayo.
Gari aina ya Land Cruiser Hardtop yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania 151,109,042 lililokabidhiwa kwa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwaajili ya kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana na
mradi wa Military HIV Research Program (MHRP) umetumia Shilingi 151,109,042
kununua gari aina ya Land Cruiser Hardtop kwaajili ya shughuli zinazohusiana na
mapambano dhidi ya Ukimwi.
Gari hiyo ambayo alikabidhiwa kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Bw.Msongela Palela na mkuu wa mkoa
wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo imenunuliwa kutokana na fedha zilizovuka mwaka
2016/2017 ikiwa ni makubaliano baina ya katibu tawala na mradi juu ya fedha
zilizovuka mwaka kupangiwa matumizi yanayolenga kuboresha huduma za Ukimwi.
Wakati akikabidhi gari hiyo Mh. Wangabo
alitahadharisha matumizi ya gari hiyo huku akipiga mfano wa gari ya Mpango wa
Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) ya halmashauri ya Wilaya ya Kalmabo iliyokuwa na
mazoea ya kwenda kwenye sehemu za starehe kuwa mshauri wa mradi huo tayari
ameshachukuliwa hatua za kinidhamu.
“Tarehe 7 mwezi wa 10 gari hii tulilishika hapa
Sumbawanga likiwa eneo la starehe na huyo mshauri wa mradi huo ndiye aliyekuwa
anaendesha gari hilo, tulichukua hatua kali za kumuondoa na kumrudisha kwa
mwajiri wake kwaajili ya hatua nyingine za kinidhamu, nitoe wito kwa madereva
wa serikali kutumia magari kwa mambo yao binafsi, suala hili lisijitokeze,
hatua kali zitachukuliwa,” alisisitiza.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa mradi
huo Bw. Riziki Kasimu ameshukuru ushirikiano anaoupata kutoka katika
halmashauri na serikali ya Mkoa ili kuhakikisha wanashusha na kutokomeza
maambukizi ya Ukimwi na ameiomba serikali ya Mkoa wa Rukwa kutoa kipaumbele kwa
kazi za Ukimwi katika matumizi ya gari.
“Pamoja na Kazi zote zilizopo Mkoani, tungependa
kazi za mradi zipewe kipaumbele katika matumizi ya gari, ni kweli kwamba tuna
kazi nyingi ama majukumu mengi ambayo hayo magari yangepaswa kufanya na sisi
kama washirika kwenye maendeleo hatuwezi kusema gari hili litumike moja kwa
moja kwa Ukimwi tu, lakini pale tunapokuwa na majukumu ya msingi ya Ukimwi
tungependa msisitizo utolewe huko,”Alisema.
Mtadi huo tayari umeshatoa gari 7 katika Mkoa wa
Rukwa, 4 katika Halmashauri zote za Mkoa na 3 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa
jambo lililosaidia kurahisisha shughuli za kupambana na maambukizi ya Ukimbwi
na hatimae kushuka kutoka asilimia 6.2 mwaka 2015 hadi asilimia 4.4 mwaka 2018.
0 comments:
Post a Comment