Waziri wa Madini, Angellah Kairuki akihutubia Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini mbalimbali (hawapo pichani) jijini Dodoma alipokuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Uchanguzi wa FEMATA jijini Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2018.
Wachimbaji wa Madini na wafanyabiashara wa madini wakiwa katika Mkutano Mkuu wa FEMATA uliofanyika katika hoteli ya African Dreams jijini Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2018.
Na Rhoda James- Dodoma
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki ameagiza Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa
Madini (FEMATA) kuhakikisha kuwa wanakuja na Mikakati ya pamoja ya kuboresha
utendaji kazi katika Sekta ya wachimbaji wadogo na kuweka mfumo bora wa kulipa
Kodi za Serikali.
Waziri
Kairuki, ameyasema haya jana tarehe 30 Oktoba, 2018 alipokuwa akifunga Mkutano
Mkuu wa Uchanguzi wa Viongozi wa FEMATA
uliofanyika katika Hoteli ya Afrikan Dreams jijini Dodoma.
Kairuki
amesema kuwa, Ukilinganisha wachimbaji wakubwa kwa wadogo nchini, wakubwa ni
asilimia nne tu wakati wachimbaji wadogo ni asilimia 96 lakini ukitazama
mchango wao kwa Pato la Taifa ni kinyume chake.
“Tunataka
FEMATA mshiriki kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanachangia kikamilifu
katika Pato la Taifa,” alisema Kairuki.
Akizungumza
katika Mkutano huo, Kairuki aliwataka wajumbe wote kutumia vyema furasa hiyo
katika kujadili na kupanga mikakati itakayotekelezwa na kuimarisha Vyama vya
wachimbaji wadogo Kimkoa (REMAS), FEMATA na hatimaye kuimarisha wachimbaji
wadogo wa madini nchini.
Aidha,
Waziri Kairuki amewapongeza FEMATA kwa kuandaa mkutano huo na kwa kutoa ushirikiano
kwa Wizara ya Madini na kuhaidi kuwa atafanya kazi kwa karibu zaidi nao na
nimatumaini yake kuwa ifikapo 2025 Sekta ya Madini itachangia ailimia isiyopungua10
ukilinganisha na mchango wa sasa ambao ni asilimia 4.8 kwa Pato la Taifa.
Akitoa
pongezi kwa Uongozi wa FEMATA, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge alieleza
kuwa ni matumaini yake kuwa wachimbaji na Wafanyabiashara wa madini wataendelea
kulipa kodi zote serikalini kama inavyotakiwa.
Kwa
upande wake, Rais wa Wachimbaji wa madini nchini John Bina amesema kuwa,
atasimamia kikamilifu ulipaji kodi, uchimbaji salama na endelevu kupitia FEMATA.
Waliohudhuria
mkutano huo ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, Manaibu mawaziri wa Madini,
Stanslaus Nyongo na Dotto Biteko, Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge,
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Viongozi mbalimbali kutoka
Serikalini ikiwa ni pamoja na Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mazingira (NEMC),
Wakala wa Usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA), Shirika la Umeme Nchini
(TANESCO), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Benki Kuu (BOT) pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wachimbaji na
Wafanyabiashara wa madini.
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) akifurahia jambo na Wanawake wachimbaji
pamoja na Manaibu Mawaziri wa Madini, Stanslaus Nyongo pamoja na Dotto Bito (wa
pili kulia na wa kwanza kushoto). Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge (wa pili kushoto), Rais wa FEMATA aliyeteuliwa
John Bina (wa tatu kulia) na mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula
(wa kwanza kulia kwa waliokaa).
0 comments:
Post a Comment