Kwa kuwa
vijana ndio nguvu kazi ya taifa ni vema kuwajengea misingi mizuri ya kupenda
kujitolea kwa ajili ya jamii yao, Na ndio maana Foundation for Civil Society
imeweza kuandaa mashindano kwa ajili ya vijana kutoa stori zao za namna walivyoweza
kijitoa katika kusaidia jamii na mwisho kuwapa zawadi wenye story nzuri zaidi.
Hayo
yamesemwa mapema jana na Afisa Uhusiano, Biashara na Maendeleo wa Taasisi ya
Foundation for Civil Society Martha Olotu wakati akiongea na waandishi wa
habari kwa Niaba ya Mkurugenzi wa FCS Bw. Francis Kiwanga katika Jumanne ya
Kutoa (Giving Tuesday), ambapo kwa mwaka huu wameweza kutoa misaada katika
kituo cha New Hope for Girls Center kilichopo kimara jijini Dar es salaam.
Akielezea
sababu za kuchagua kituo hicho afisa huyo amesema ni moyo wa upendo na
wakujitolea alionao huyo Mama kwa kuwachukua mabinti wanaoishi katika mazingira
hatarishi, Yatima, na walioterekezwa na familia zao na kuamua kuishi nao
nyumbani kwake wakiwa ni kama sehemu ya familia yake na sio kama watoto ambao
wapo kwenye kituo cha kulelewa.
Aliongeza
kuwa mbali na tukio hilo la kuandaa mashindano kwa vijana, lakini pia kampeni
hiyo ilitanguliwa na tukio la kijitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa
mbalimbali wenye uhitaji wa damu katika Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha MOI
ambapo watu 38 waliweza kijitolea damu.
Aidha aliendelea
kusema kuwa wametoa misaada yenye thamani ya zaidi ya Milioni Kumi hii ikiwani
FCS, wananchi mbalimbali, pamoja na mashirika mengine yaliyoguswa na tukio
hilo, lakini kwa wafanyakazi wa Foundation for Civil Society wamejichanga na
wametoa mashine ya Photocopy ikiwa ni kama njia ya kuacha alama katika kituo hicho.
Kwa upande
wake Mama mlezi wa wasichana hao Bi. Consoler Eliya alisema kuwa sababu
iliyomsukuma kufanya hivyo ni kutokana na ugumu wa maisha pamoja na mazingira hatarishi
ambayo ameyapitia wakati akiwa msichana, Ikiwa ni pamoja na kupigwa sana, kukosa
nafasi ya kusoma kutokana na magonjwa yaliyotokana na kipigo cha mara kwa mara.
Aliendelea kusema
kuwa kutokana na vipigo ilifikia hata kwenda kufanyiwa upasuaji mara kadhaa, kulazwa stoo ya uchafu na kuamshwa kwa kumwagiwa maji, kufedheheshwa
kwa maneno na matusi hali iliyosababisha kuishi kama omba omba mtaani na hata
kulazimishwa kuolewa akiwa na umri wa miaka 11, na baada ya hayo yote alipiga
goti kwa mungu na kumuomba akimsaidia atakuwa ni mama kwa watoto wanaoishi
katika mazingira magumu kama aliyopitia yeye.
Na kwa
kumtegemea mungu aliweza kuvushwa katika majaribu hayo na ndipo alianza kumlea mtoto
wa kwanza akiwa bado ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa kutumia Boom
lake, na alipomaliza chuo alikuwa na wasichana saba na mpaka sasa yeye na mumewe
wanawahudumia wasichana 40 na wawili wakiwa ni watoto wao wa kuwazaa wenyewe.
Naye Janeth
Thobias ambaye ni miongoni mwa wasichana wanaolelewa na Mama huyo alisema kuwa
sababu ya wao kuonekana ni wenye Amani na Furaha, ni kutokana na mafundisho mazuri
anayowapatia na kila siku, lakini pia upenda kuwasihi wasahau yale
waliyofanyiwa hapo nyuma eidha na ndugu au walezi wao na kuwakumbusha mara kwa
mara kuwa silaha pekee itakayowakomboa katika maisha yao ni upendo.
Aliendelea kusema
kuwa sababu nyingine ni malezi mazuri wanayopatiwa na Mama huyo, kwa kuishi nao
kama sehemu ya familia yake na mara kwa mara anawasisitiza kuhusu umuhimu wa
elimu na kuwataka wasome kwa bidii kwa kuwa elimu ndio msingi wa maisha yao.
Afisa Uhusiano, Biashara na Maendeleo wa Foundation for Civil Society Martha Orotu akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema jana jijini Dar es salaam katika siku ya Jumanne ya Kutoa (.Giving Tuesday).
Msichana Janeth Thobias ambaye ni miongoni mwa mabinti wanaolelewa katika kituo hicho akisoma Risala mbele ya wageni waalikwa mapema jana jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wasichana wa kituo cha New Hope for Girls Center wakiimba shairi mbele ya wageni waalikwa.
Edna Chilimo kutoka Foundation for Civil Society akiongea na Wasichana wa kituo cha New Hope for Girls Center.
Baadhi ya zawadi zilizotolewa kwa kituo hicho.
Zawadi nyinginezo.
Baadhi ya wasichana wa kituo cha New Hope for girls Center wakionyesha maonyesho ya mavazi mbele ya wageni waalikwa.
Baadhi ya washiriki wa Jumanne ya kutoa wakifuatilia matukio yanayoendelea katika tafrija hiyo.
0 comments:
Post a Comment