Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo wakati alipowasili kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salam
kushiriki katika Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Watu wa
Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuuheshimu na
kuuendeleza utamaduni ambao ndio urithi wao ili kulifanya Taifa liendelee kuwa
hai.
Amesema
suala la kuuenzi utamadini ni jambo zuri ambalo linatoa fursa kwa watu wengine
hususan wa mataifa ya nje kuja kujifunza historia ya Watanzania na maisha yao.
Waziri Mkuu
aliyasema yao jana jioni (Ijumaa, Oktoba 26, 2018) alipotembelea shughuli za
tamasha la utamadini wa Mtanzania kwa jamii ya watu wa Lindi.
Katika
tamasha hilo linalofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam,
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania waendelee kuupenda
utamaduni wao.
“Nimefurahi
kuona nyumba zikiwa na zana mbalimbali za kitamaduni ambazo zilikuwa zikitumiwa
na wazee wetu pamoja na namba ya utayarishaji wa vyakula vyetu vya asili.”
“Sikutarajia
kuona haya ninayoyaona, nawashukuru wote walioshiriki katika kandaa tamasha hili
pamoja na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Kijiji cha Makumbusho.”
Waziri Mkuu
alisema tamasha hilo ambalo limewakutanisha Wanalindi kutoka katika wilaya
mbalimbali linatoa fursa ya wao kujadili maendeleo ya mkoa wao na Taifa kwa
ujumla.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwaomba wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda katika Kijiji
cha Makumbusho kwa ajili ya kujifunza historia ya mkoa wa Lindi pamoja na fursa
zilizoko.
Awali, Mkuu wa
Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema mkoa umetumia tamasha hilo kutoa
ujumbe kwa umma kuhusu vivutio mbalimbali walivyonavyo pamoja na fursa za
uwekezaji.
0 comments:
Post a Comment