METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, October 21, 2018

TANZIA: WATUMISHI WATANO WA WIZARA YA KILIMO WAFARIKI KWA AJALI

Na Mathias Canal, WK

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe anapenda kuwataarifu watanzania kuwa Wizara ya Kilimo imepatwa na msiba wa Watumishi wake Watano (5).

Watumishi hao wamepatwa na mauti kwa ajali ya gari iliyotokea leo asubuhi tarehe 21 Oktoba, 2018 Wilayani Manyoni katika Mkoa wa Singida, wakiwa safarini kuelekea Mkoani Mwanza kikazi. 

Watumishi hao waliofariki ni;

1. Stella Joram Ossano (39)

2. Esta Tadayo Mutatembwa (36) 

3. Abdallah Selemani Mushumbusi (53)

4. Charles Josephat Somi (32)

5. Erasto Mhina (43)

Tayari miili ya marehemu imewasili katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo tarehe 21 Oktoba 2018.

Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi, AminaπŸ™πŸΏ

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com