Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji na kata ya Bukyaheke akiwa kwenye ziara ya siku moja ya kikazi katika jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza kukagua shughuli za utekelezaji wa ahadi alizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka 2015, jumapili tarehe 21 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua ujenzi wa soko la kisasa la samaki wakati akiwa kwenye ziara ya siku moja ya kikazi katika jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza kukagua shughuli za utekelezaji wa ahadi alizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka 2015, jumapili tarehe 21 Octoba 2018.
Sehemu ya wananchi wa kijiji na kata ya Bukyaheke wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati akiwa kwenye ziara ya siku moja ya kikazi katika jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza kukagua shughuli za utekelezaji wa ahadi alizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka 2015, jumapili tarehe 21 Octoba 2018.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Bukyaheke wakati akiwa kwenye ziara ya siku moja ya kikazi katika jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza kukagua shughuli za utekelezaji wa ahadi alizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka 2015, jumapili tarehe 21 Octoba 2018.
Na Mathias Canal,
Bulyaheke-Mwanza
Mbunge wa Jimbo la Buchosa
Mkoani Mwanza Mhandisi Dkt Charles Tizeba jumapili tarehe 21 Octoba 2018
alifanya ziara ya siku moja ya kikazi katika jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza
kukagua shughuli za utekelezaji wa ahadi alizozitoa kwenye kampeni za uchaguzi
Mkuu mwaka 2015.
Pamoja na mambo mengine katika
ziara hiyo Dkt Tizeba alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kuendelea
kuiamini serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe
Magufuli.
Pongezi hizo pia zinatuama
kuwashukuru wananchi kwa kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwa kumchagua Rais,
Mbunge na madiwani wanaotokana na CCM.
Akihutubia kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Bukyaheke Dkt Tizeba amechangia
jumla ya shilingi Milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho
sambamba na kuchangia mifuko 100 ya saruji.
Vilevile, Mbunge huyo amewataka
wananchi kushiriki katika shughuli za ujenzi wa zahanati hiyo ambapo pindi boma
litakapokamilika atachangia mabati yote yatakayohitajika kwa ajili ya kuezeka.
Dkt Tizeba alisema kuwa lengo la
kuchangia mahitaji hayo ni kuakisi ahadi ya ujenzi wa zahanati katika kila
kijiji ili kuboresha huduma za upatikanaji wa tiba kwa wananchi katika vijiji.
Mchango huo pia umejibu
changamoto iliyoainishwa kwenye taarifa fupi ya kijiji na Afisa Mtendaji wa
Kijiji cha Bulyaheke Ndg Ezekiel Galula aliyeomba mchango wa mbunge huyo
kufabikisha ujenzi wa zahanati.
Dkt Charles Tizeba ambaye ni
Waziri wa kilimo amewataka wananchi hao kununua haraka dawa za kuua wadudu
vamizi kwenye Mazao kwani kutofanya hivyo kutasababisha wadudu hao kuvamia
mashamba yote.
Katika hatua nyingine Dkt Tizeba
amepiga marufuku walimu kuwatumia wanafunzi kulima kwenye mashamba yao pamoja
na kufanya shughuli binafsi za walimu huku akisisitiza kuwa kwa mashamba ambayo
ya walimu ambayo tayari yamelimwa na
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment