Bi. Halima Mpita (Kulia) akitoa ufafanuzi juu ya matumizi ya mkaa wa
makaa ya mawe kwa wadau mabalimbali waliohudhuria katika semina
hiyo.
Mkaa wa mawe unavyowaka.
Mkoa wa Rukwa
umejipanga kupambana na uharibifu wa mazingira kwa kuhakikisha wanatumia
rasilimali za makaa ya mawe yanayopatikana katika kijiji cha Nkomolo tu, Wilayani
Nkasi kuwa mkaa mbadala na kuanza kutumika majumbani.
Mkakati huo
ulioanza kwa mafunzo ya siku mbili yaliyoendeshwa na mtaalamu wa makaa hayo
kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe bi. Halima Mpita ukiwakutanisha
makatibu tawala wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, madiwani, wataalamu wa
mazingira kutoka katika halmashauri, mashirika yasiyo ya kiserikali
yanayoshughulikia mazingira pamoja na wazee maarufu.
Akiongea
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya nishati mbadala inayotokana na makaa ya mawe
mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachima Wangabo amesema kuwa tunafanya kila
liwekanalo kuokoa kile kilichopo na kuhakikisha kwamba mazingira hayaendelei
kuharibiwa kwa namna yoyote hasa masuala ya kukata miti kwaajili ya kuni na
mkaa.
“Makaa ya
mawe yapo kilomita 45 toka hapa tulipo (sumbawanga mjini), yale makaa yam awe
tunaweza kuyatumia kama mkaa mbadala kwa matumizi ya majumbani, na hili ndio
lengo la mafunzo ya leo, mtaalamu wetu atatueleza kule Songwe wanafanyaje, kile
wanachofanya kule watatumegea hapa uzoefu wao, na sisi tutaona na kujipanga
tufanye nini na haya makaa yam awe tuliyonayo,” Alisema.
Ameongeza
kuwa endapo mafanikio yatapatikana na kuanza kutumia makaa ya mawe majumbani,
kiwango kikubwa cha uvunaji wa miti kitaokolewa na kutahadharisha kuwa mpango
huo ukifanikiwa gharama za kununua bidhaa hiyo isiwakatishe tamaa wanunuzi ili
wasirudi tena kukata miti na hatimae kutofikia lengo.
Kwa upande
wake Bi. Mpita alisifu muitikio wa wadau wa mazingira wa mkoa wa Rukwa na
kusema kuwa endapo nguvu hiyo itafikisha elimu kwa wananchi basi mkoa wa Rukwa
utakuwa wa kuigwa na kuongeza kuwa atashirikiana bega kwa bega ili kuhakikisha
mafanikio yanapatikana kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.
Akieleza
faida za mkaa unaozalishwa na makaa yam awe alisema, “Haya makaa ni suluhisho
la kudumu juu ya matumizi mbadala la mkaa wa miti kwa kuwa miamba ya makaa ya
mawe ni ya asili na inaweza kuvunwa zaidi ya miaka 500. Pia unaweza kuwaka kwa
saa 3 hadi 4 mfululizo na hautoboi wala kuchafua sufuria, ni mkombozi wa
ajira maana uanzishaji wa kiwanda chake ni rahisi na majivu yake hustawisha
mimea,” Alisisitiza.
Ili kuuwasha
Mkaa wa makaa ya mawe unahitaji jiko la mkaa lililotengenezwa kwa udongo,
utawasha vijiti viwili maalum vya kuwashia moto utaweka vipande 4 hadi 5 acha
viwake pamoja kwa dakika 3, ongeza mkaa na uache uko kwa dakia 15 hadi makaa
ubadilike na kuwa rangi nyekundu kuanzia chini. Vipande 34 vya mkaa vinatosha
kumaliza mapishi ambapo mkaa huo huwaka kwa masaa 3 hadi 4.
0 comments:
Post a Comment