METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, October 25, 2018

MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA CHALINZE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Chalinze waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Polisi Chalinze ikiwa sehemu ya ziara yake ya kugagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Lugoba ambapo Makamu wa Rais alikagua ujenzi wa kituo cha Afya Lugoba ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku zita mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema atamuagiza Waziri wa Kazi kufanya ziara kwenye Viwanda mkoani Pwani kusikiliza kero za wafanyakazi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati akihutubia wakazi wa Chalinze kwenye uwanja wa Chalinze Polisi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.
“Nimesikia nong’ono kuna tatizo la maslahi ya wafanyakazi wanaofanya kazi viwandani sasa hivi lakini nataka niwaahidi kwamba hili nitakwenda zungumza na Waziri wa Kazi afanye ziara ya kupita viwandani ili asikie malalamiko ya wafanyakazi katika viwanda vile” alisema Makamu wa Rais.
Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alisisitiza ahadi ya kuondoa tatizo la maji kwa wananchi wa Chalinze ipo pale pale kwani Serikali ya awamu ya tano imeweka jitihada kubwa kuhakikisha inaondoa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, pia alitoa rai kwa vijana kujifunza ufundi na kuongeza elimu ili wawe na sifa za kuajirika, pia alihimiza wananchi wa Chalinze kujiandikisha kwenye mfuko wa Bima ya Afya.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete alimueleza Makamu wa Rais kuwa Halmashauri ya Chalinze inafanya kwa vitendo kutafsiri ahadi ya Mheshimiwa Rais pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 ambapo amesema Chalinze imefungua milango kwa wawekezaji wa aina zote.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com