Dkt Charles Tizeba Waziri wa kilimo akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi maalumu ya kujitolea kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza leo tarehe 25 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Dkt Charles Tizeba Waziri wa kilimo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela wakikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza wakati walipotembelea kambi maalumu ya vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga walioamua kufanya ujenzi kwa kujitolea, wakati akiwa safarini kuelekea Wilayani Korogwe leo tarehe 25 Septemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo katika kambi maalumu wakijitolea katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza leo tarehe 25 Septemba 2018.
Na Mathias Canal-WK,
Muheza-Tanga
Imeelezwa kuwa sehemu pekee ya
kuimarisha kilimo cha mwananchi mmoja mmoja, wananchi katika makundi ya kijamii
hususani vijana ni kupitia sekta ya kilimo kwani ndio sehemu pekee ya ukombozi
wa mkulima katika jamii.
Imeelezwa kuwa kuna uwezekano wa
kufanya biashara mbalimbali nchini ambazo zinaweza kuongeza kipato lakini
sahemu sahihi isiyokuwa na jazba na dhoruba katika utendaji ni kufanya kilimo
biashara ambacho kamwe hakiwezi kumtupa mkulima.
Dkt Charles Tizeba Waziri wa
kilimo, ameyasema hayo leo tarehe 25 Septemba 2018 wakati akizungumza na vijana
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga ambao wapo
katika kambi maalumu ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza.
Vijana hao ambao wameamua
kutumia nguvu zao pasina malipo wameamua kwa umoja wao kuunga mkono juhudi za
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kauli yake inayohamasisha chachu na
juhudi za kiutendaji kwa wananchi ya "Hapa Kazi Tu".
Aidha, katika kuhamasisha juhudi
za kiutendaji Waziri huyo mwenye dhamana ya kilimo ameunga mkono juhudi za
vijana hao kwa kuchangia fedha ya chakula shilingi 1,100,000 sambamba na
kushiriki ujenzi wa jengo maalumu la upasuaji.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles
Tizeba alitembelea ujenzi huo wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza akiwa safarini
kutembelea mashamba ya mkonge ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya kikazi Mkoani
Tanga aliyoianza jana tarehe 25 Septemba 2018 ya kukutana na makundi
mbalimbali ya wakulima wa zao la Mkonge ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto
zinazowakabili wakulima wa zao hilo.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment