METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 25, 2018

DKT TIZEBA AMUAGIZA MKURUGENZI BODI YA MKONGE KUWACHUKULIA HATUA WAVAMIZI WA MASHAMBA YA MKONGE

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo kijijini Lwengela kata ya Kwa Gunda wakati akizungumza na wakulima wa Mkonge katika shamba la Magunga lililopo Wilayani Korogwe Leo tarehe 25 Septemba 2018 akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa Mkonge kwenye shamba la Hale lililopo katika Kata ya Hale wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo tarehe 25 Septemba 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela akieleza malalamiko ya wananchi dhidi ya kampuni ya Katani Ltd mbele ya Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba katika mkutano na wakulima wa Mkonge kwenye shamba la Hale lililopo katika Kata ya Hale wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo tarehe 25 Septemba 2018.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lwengela kata ya Kwagunda wakifatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza na wakulima wa Mkonge katika shamba la Magunga lililopo Wilayani Korogwe Leo tarehe 25 Septemba 2018 akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga.

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza na wakazi wa kijiji na kata ya Magoma ambao ni wakulima wa Mkonge katika shamba la Magoma Wilayani Korogwe mkoa wa Tanga tarehe 25 Septemba 2018.

Na Mathias Canal-WK, Korogwe-Tanga

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba Leo tarehe 25 Septemba 2018 amemuagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Ndg Yunus Msika kuwachukulia hatua za kisheria wote waliobainika kuvamia mashamba ya wakulima wa Mkonge.

Alisema kitendo cha kuvamia mashamba ya wakulima na kuvuna Mali zao kisha kwenda kuuza ni wizi kama ulivyo ubadhilifu mwingine wa kuharibu mali za wananchi hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa wale wote watakaobainika katika kadhia hiyo.

Waziri Tizeba ametoa agizo hilo wakati wa muendelezo wa ziara yake Mkoani Tanga wakati akizungumza na wakulima katika mikutano ya hadhara katika katika Kijiji cha Hale, Lwengela na kijiji cha Magunga mara baada ya kutembelea mashamba ya Hale, Magunga na Magoma.

"Mkurugenzi wa Bodi nitashangaa sana kama kuna watu wamevamia mashamba ya wakulima wakakata Mkonge ukiwa shambani tena bila makubaliano yoyote na wahusika na kwenda kuuza jambo hilo ni kinyume kabisa na utaratibu watu hawa wakamatwe haraka iwezekanavyo na haki za wakulima zipatikane" Alikaririwa Dkt Tizeba na kuongeza kuwa

" Hilo ni kosa la jinai kabisa halipaswi tu kupelekwa mahakama ya ardhi au mabaraza ya kata bali linapaswa kuchukuliwa uhalali kweli kweli watu wawajibike bila masihara" 

Katika hatua nyingine waziri huyo amewakumbusha wakulima hao kuwa migogoro inayoendelea kati yao na kampuni ya Katani ltd sasa inapaswa kufikia ukomo endapo suluhu itashindwa kupatikana serikali italazimika kuvunja mkataba kwani wapo wananchi, taasisi na makampuni binafsi mengi yanataka kuwekeza katika kilimo cha zao hilo la Mkonge.

Katika hatua nyingine Waziri Tizeba amemuagiza Afisa kilimo wa Wilaya ya Korogwe kuandaa ratiba ya kazi ya Wilaya na kumpatia Mkuu wa Wilaya hiyo ili maaafisa ugani wa kata waweze kuwajibika ipasavyo.

Awali akitolea ufafanuzi kuhusu malalamiko ya wananchi Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Yunus Msika alisema kuwa tayari Bodi hiyo imeunda Tume maalumu ili kubaini wabadhilifu hao na kuchukuliwa hatua stahiki ambapo kwa hivi sasa inajiridhisha kiasi cha mashamba yaliyovaMkonge.a gharama zilizopotea.

MWISHO.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com