METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 27, 2018

DKT TIZEBA ATANGAZA NEEMA KWA WABANGUAJI WADOGO WA KOROSHO

Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza na Umoja wa wabanguaji wadogo wa korosho Tanzania (UWWKT) katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini Dar es salaam juu ya kujadili mwenendo wa ubanguaji wa korosho leo tarehe 27 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Muwakilishi wa Chama cha wabanguaji wakubwa wa korosho ( Cashewnuts Prossors Association) Ndg Peter Christopher akisoma taarifa ya chama hicho mbele ya waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini Dar es salaam juu ya kujadili mwenendo wa ubanguaji wa korosho leo tarehe 27 Septemba 2018. 
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na Umoja wa wabanguaji wadogo wa korosho Tanzania (UWWKT) katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini Dar es salaam juu ya kujadili mwenendo wa ubanguaji wa korosho leo tarehe 27 Septemba 2018. Mwingine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Prof Wakuru Magigi.
Mwenyekiti wa Umoja wa wabanguaji wadogo wa korosho (UWWKT) Bi Tumpale Salum Magehema akisoma taarifa ya umoja huo mbele ya waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano kwenye uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini Dar es salaam juu ya kujadili mwenendo wa ubanguaji wa korosho leo tarehe 27 Septemba 2018. 

Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam

Korosho ni moja ya mazao makuu ya biashara nchini. Kwa sasa zao la korosho linalimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania, yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma, Pwani na Tanga ambapo kwa kiasi Fulani mkoani Singida wakulima pia wameamka kimkakati kwa kuanza kujikita katika kilimo hicho.

Kuelekea uchumi wa viwanda nchini, serikali imesema kuwa itafanya mazungumzo ya haraka na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuboresha zaidi huduma sambamba na kufikia wakulima wengi kwa kuwapa mikopo ili kuinua sekta ya kilimo ambayo ndiyo mtoaji wa malighafi zinazotumiwa na viwanda hivyo.

Pamoja na zao hilo kuwa sehemu ya mhimili mkubwa wa uchumi wa wakulima na Taifa kwa ujumla, bado wabanguaji wadogo wa korosho nchini wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa elimu ya ubanguaji wenye tija ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji jambo linalopelekea wabanguaji hao kukosa sifa ya kukopesheka.

Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba leo tarehe 27 Septemba 2018 ametangaza neema kwa wabanguaji wadogo wa korosho kwa kuitaka benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kuwawezesha wabanguaji hao mikopo yenye masharti nafuu ili kuwa na mitaji itakayopelekea kuongeza tija katika ubanguaji wa korosho nchini.

Waziri Tizeba ameyasema hayo wakati akijibu maoni na mapendekezo yaliyosomwa kwenye taarifa ya Umoja wa wabanguaji wadogo wa korosho Tanzania (UWWKT) katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano katika uwanja wa kimataifa wa michezo (National Stadium) Jijini Dar es salaam.

Ili kuongeza ufanisi na tija katika ubanguaji chama hicho kimeishauri serikali kutoa elimu ya ubanguaji ili kupata bidhaa bora yenye kukidhi viwango vya soko la Kimataifa na kuwezesha upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu kwani kufanya hivyo wabanguaji hao wadogo wataweza kuongeza uzalishaji kutoka Tani 64 kwa mwaka hadi kufikia Tani 192 kwa mwaka.

Dkt Tizeba aliagiza kutazamwa upya mfumo wa stakabadhi ghalani ili kurahisisha ununuzi wa korosho kwani kwa sasa unamtaka mnunuzi kununua kuanzia tani 50 jambo linalofanya wabanguaji wadogo kushindwa kuingia katika soko hilo.

Alisema kuwa Sekta ya kilimo nchini ni kitovu cha maendeleo ya viwanda kwa kutoa masoko na malighafi za viwandani ambapo inaajiri Watanzania wengi takribani zaidi ya asilimia 67.

Katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo, Serikali inaendelea kuimarisha mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya kilimo ikiwemo kuimarisha masoko ya kilimo ili sekta hiyo iendelee kuwa na tija kwa wakulima nchini na taifa kwa ujumla.

Alisema ili kuongeza ufanisi na tija Serikali katika mwaka wa fedha 2017/2018 imefuta ada na tozo zipatazo 80 kati ya tozo na ada 139 zilizokuwa zinatozwa katika mazao ya kilimo nchini ambazo zilibainika kutokuwa na tija kwa wakulima.

Katika kurahisisha utendaji kwenye zao la korosho Serikali imefuta tozo tano kati ya tisa alizokuwa anakatwa mkulima wa zao la Korosho baada ya kubainika kwamba hazikuwa sahihi.

MWISHO.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com