Waziri wa Kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania tawi la Mtwara tarehe 29 Septemba 2018.
Na Mathias Canal-WK,
Mtwara
Uwepo wa mfumo wa
stakabadhi ghalani umekuwa ni mkombozi pekee kwa wakulima wadogo na wa kati kwa
kuwawezesha kupata bei nzuri ya mazao yao, ukilinganisha na bei zilizokuwa
zinatolewa na wafanyabiashara wanaponunua mazao yakiwa shambani kwa kutumia
vipimo ambavyo sio sahihi.
Kabla ya mfumo huo kuanza wakulima walikuwa wakipunjwa bei ya mazao na wafanyabiashara ambapo hata hivyo kumekuwepo na mwamko miongoni mwa wakulima, kupitia vyama vyao vya msingi, wa kutumia mfumo halisi wa stakabadhi ghalani pasipo kuchukua mikopo toka Taasisi za Fedha. Katika msimu wa mwaka 2017/2018 vyama vyote viliweza kukusanya na kuuza mazao bila kukopa benki.
Hayo yamebainishwa tarehe 29 Septemba 2018 na
Waziri wa Kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akifungua Mkutano
Mkuu wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Benki kuu ya Tanzania tawi la Mtwara.
Alitaja kuwa ushirika ni dhana
ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana, Dhana hiyo imefanikiwa kuleta mabadiliko
ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita ambapo uanzishwaji wa vyama vingi vya ushirika kwa
sasa unatokana na elimu watu wengi waliyoipata kuhusu Ushirika. “Ni wazi kuwa katika
kipindi cha miaka miwili hivi, imani kwa vyama vya ushirika imeongezeka na
vyama vingi vinaendelea kuundwa hasa vile vya kuweka na kukopa, yaani SACCOS”
Alikaririwa Dkt Tizeba
Dkt Tizeba alitoa wito kwa vyama vya ushirika
kuendelee kukusanya korosho kwa msimu huu ili soko na bei iendelee kuwa imara
pamoja na kuwa na misuko suko mingi ya masoko Duniani. “Aidha ni vyema Wakulima
wote wakajiandisha na kuwa Wanachama wa vyama vya Ushirika amabpo watapata
faida nyingi ikiwemo kufanya maamuzi kwa pamoja” Alisema Dkt Tizeba
Alitaja mafanikio katika zao hilo kuwa ni
pamoja na kuimarishwa kwa usimamizi wa zao, uratibu mzuri wa ununuzi na
usambazaji wa pembejeo za ruzuku, usimamizi wa karibu unaofanywa na viongozi wa
serikali katika ngazi zote, na hamasa mpya ya wakulima kujishughulisha na
kilimo cha korosho katika maeneo asilia na maeneo mapya.
Dkt Tizeba alisisitiza kuwa hali hiyo
ikiendelea kuna uwezekano wa kuzalisha zaidi ya kiwango cha sasa na kuwa na
malighafi inayoweza kutumika kwa mwaka mzima kwa kuuza nje na viwanda vya ndani.
Katika hatua nyingine aliongeza kuwa pamoja na
kuwa na mafanikio makubwa kwenye zao la korosho lakini zipo changamoto
mbalimbali ambazo ni pamoja na kuwepo kwa mashamba makubwa ya mikorosho
iliyotelekezwa, Uchelewashaji wa malipo kwa Mkulima, Wanunuzi kulalamikia
upotevu wa Korosho, ubora hafifu na ubadhilifu, pamoja na Ucheleweshaji wa
malipo toka wa Mabenki kwenda vyama na uwepo wa suspence account ambazo zinaathiri malipo kwa Mkulima.
Hivyo katika kufanikisha na kuwa na maendeleo
katika zao hilo yanatakiwa kufanyika mabadiliko ambayo yatahitaji ushirikiano wa
wadau na hasa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika usimamizi
ili kuhakikisha Mkulima anapata fedha kwa Wakati.
Ameelekeza kuwa katika msimu huu kila Halmashauri
ianzishe sehemu maalumu ya Malipo kwa Wakulima (Payment centre) ambapo
wataalamu watasaidia vyama hususani toka Vyama Msingi kwenda kwa Wakulima baada
ya ukokotoaji wa gharama mbalimbali na kupeleka benki kwa wakati jambo ambalo
litasaidia kubaini mapungufu ya kimalipo kwa mabenki na au unaosababishwa na
Watendaji wa Vyama.
Waziri Tizeba pia ameelekeza kuwa, Mtiririko
wa Malipo kwa Mkulima unapaswa kusimamiwa vizuri na kila Halmashauri ya Wilaya
iwe na kituo kitakachorahisisha malipo kwa Mkulima mara baada ya fedha kutoka
Chama Kikuu cha Ushirika kwenda AMCOS (Payment Clinc Centre), Secretatiati za
Mikoa, Halmashauri, Kamati za Ulinza, Bodi ya Korosho, Mrajis wa Vyama
vya Ushirika na mabenki kushirikiana kuhakikisha jambo hilo linatekelezeka ili
kumpunguzia Mkulima adha ya Malipo
MWISHO
0 comments:
Post a Comment