Na Asteria Muhozya, Simanjiro
Waziri wa Madini Angellah Kairuki
amesema anaona fahari kutokana na uwekezaji wa Kiwanda cha Kuchakata madini ya
Kinywe (Graphite) uliofanywa na Kampuni ya wazawa ya GOD Mwanga Gems Ltd
iliyopo Kata ya Endiamtu, Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.
Waziri Kairuki ameyasema hayo leo
tarehe 2 Agosti, alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujionea shughuli
zinazofanywa na kiwandani hapo.
Amesema Serikali imekuwa ikihamasisha
waombaji wa leseni za madini kuwekeza katika maeneo mbalimbali hivyo, jambo lililofanywa
na kiwanda hicho ikiwemo malengo ya kiwanda husika kufungua viwanda vingine katika mikoa ya Tanga na
Manyara ni jambo la kujivunia na fahari kwa Tanzania.
“Nimefurahishwa sana namna kampuni hii
inavyofanya kazi. Serikali kupitia wizara yangu imekuwa ikihamasisha uwekezaji.
Tuko tayari kuwasimamia na kuwasaidia katika hili. Tunataka kutengeneza ajira
zaidi, kukuza uchumi kupitia madini lakini pia serikali kupata kodi,” amesisitiza
Kairuki.
Akijibu ombi la kampuni hiyo kupata
kibali cha kuuza madini hayo nje, Waziri Kairuki ameahidi kampuni hiyo kuwa
mara baada ya taratibu za utoaji vibali kukamilika Wizara kupitia Tume ya Madini
itatoa kibali kwa kampuni husika iendelee na taratibu zake za kuuzwa nje ya nchi madini hayo.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Kairuki
amewataka wenye leseni za madini kutozitumia leseni hizo kuziweka rehani kwa
kuwa Sheria ya Madini inakataza jambo hilo badalayake zinatakiwa kutumiwa
katika malengo yaliyokusudiwa.
“Wapo baadhi ya wawekezaji wamepewa
leseni lakini hawajafanya chochote wengine wanaweka rehani leseni hizi.
Nafurahi kuona mzawa mwenzetu amefanya jambo kubwa kama hili, leo nimejionea
uhalisia katika jambo hili,” amesema
Waziri Kairuki.
Pia, Waziri Kairuki ameishauri kampuni
husika kuendelea kuitumia Maabara ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Tanzania
(GST) kwa ajili ya shughuli za utafiti na pia kuwatumia wahitimu wa Chuo Cha
Madini Dodoma (MRI) katika suala la ajira.
Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki
amesema Wizara imewachukulia hatua watumishi 40 kutokana na kwenda kinyume na
maadili ya utumishi wa umma katika suala zima la usimamizi katika sekta husika.
“Wapo tuliowahamisha vituo vya kazi,
wengine tumewasimamisha. Tunachotaka ni kuendana na kasi na huku wakizingatia
maadili ya utumishi,” amesema Waziri Kairuki.
Aidha, amesisitiza suala la wawekezaji
kuendelea kutoa taarifa za uzalishaji ili
serikali iweze kupata kodi
zake huku akisisitiza suala la ulipaji
kodi kwa serikali na wenye leseni zao
kuzitumia na kuzalisha kwa viwango vinavyohitajika.
Kwa upande, Meneja wa Kiwanda hicho
Henry Mbando ameiomba serikali kukisaidia kiwanda hicho kupata kibali kwa ajili
ya kuuza madini hayo nje ya nchi ambayo yana masoko katika nchi za Marekani,
Kanada, China na ulaya.
Ameongeza kuwa, madini hayo yanatumika
kutengeneza bidhaa mbalimbali za
viwandani vikiwemo vipuri vya magari, betri za magari na mitambo mengine.
Ameongeza kuwa, soko la madini hayo ni
katika nchi za
Akizungumzia idadi ya wafanyakazi waliopo
kiwandani hapo amesema kiwanda kina jumla ya watumishi 80 huku waanawake wakiwa
2 na wanaume 78.
Naye, Mmiliki wa kampuni hiyo,
Godlisten Mwanga ameishukuru Serikali kwa msamaha wa kodi katika baadhi ya
mitambo aliyoinunu kwa ajili ya kiwanda hicho na pia kumshukuru waziri Kairuki
kwa kuona umuhimu wa kutembelea kiwanda husika.
Amesema kiwanda hicho kimezalisha tani
zaidi ya 2,000 na zilizotayari kwa ajili ya kuuzwa ni tani 200.
Akizungumzia suala la kibali kwa
kampuni husika Kamishna wa Madini Mhandisi David Mlabwa amesema kuwa, awali
kampuni hiyo ilikuwa haijakidhi vigezo vya kupata kibali lakini baada ya
kukidhi viwango hivyo itapatiwa kibali.
0 comments:
Post a Comment