Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) akilakiwa na mwenyeji wake Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Mb) mara baaada ya kuwasili kijijini Kangeme Kata ya Ulowa kukagua ghala la tumbaku la Chama cha msingi Kangeme. Jana 16 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maeleazo kutoka
kwa Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba. (kushoto)
wakati alipokagua uuzaji wa tumbaku katika Chama cha Ushirika cha
Msingi cha Kangeme katika Halmashauri ya Ushetu, Julai 16,
2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab
Telack na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Nchini, Dkt Titus Kamani, Jana 16 Julai 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata akimshuhudia Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba (katikati) akijaribu kuendesha pikipiki moja kati ya tatu alizomkabidhi kwa ajili ya kuimarisha sekta ya kilimo Halmashauri ya Ushetu, Julai 16, 2018. Katika hafla hiyo pia Waziri Mkuu alimkabidhi Dkt Tizeba gari aina ya Toyota Land Cruiser. Mwingine pichani ni Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb) na Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEM) Mhe Joseph Kakunda.
Na Mathias Canal,
Ushetu-Shinyanga
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Charles Tizeba katika kipindi cha miaka miwili tangu ateuliwe kuhudumu
katika nafasi hiyo kwa kupaisha zao la Korosho kutoka shilingi 1470 kwa kilo
moja au 1480 na hatimaye kufikia shilingi 4300 kwa kilo moja.
Alisema kuwa katika kipindi cha
miaka mitatu iliyopita zao hilo lilikuwa likiuzwa kati ya shilingi 700 mpaka
800 kwa kila kilo moja jambo ambalo lilimdidimiza mkulima kwani aliwekeza nguvu
nyingi katika Kilimo lakini tija ya nguvu zake ilikuwa na thamani ndogo.
Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo
jana 16 Julai 2018 kijijini Kangeme Kata ya Ulowa wakati akihutubia mamia ya
wananchi waliojitokeza kwenye sherehe za uzinduzi wa mpango wa matibabu kwa
wanachama wa vyama vya ushirika nchini unaojulikana kama Ushirika Afya.
Alitoa pongezi hizo pia kwa
waziri Tizeba kutokana na juhudi zake anazozifanya ikiwa ni pamoja na kuongezeka
maradufu kwa bei kwenye zao la ufuta kutoka shilingi 1000 kwa kilo hadi kufikia 3000 kwa kilo.
Aidha,
katika kuongeza ufanisi kwenye kuimarisha na kufanua mabadiliko ya kimazoea
katika vyama vya msingi, Waziri Mkuu alimuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Shinyanga, Simon Haule kuwakamata viongozi wa Chama cha Msingi cha Mkombozi kwa
upotevu wa dola za marekani 21,000 za chama hicho.
"Wabebe
hawa watu, wahoji waseme hiyo fedha iko wapi na jambo la kwanza wailete hiyo
fedha ya wakulima. Wakishindwa kurejesha fedha, wawekwe ndani," alisema.
Waziri
Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kuwaita viongozi wa chama cha Mkombozi watoke
hadharani na kubaini kuwa hakuwepo hata mmoja. Inadaiwa kwamba walitoroka baada
ya wananchi kuanza kuzomea.
Kamanda
Haule amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mwenyekiti, Bw. Shilinde Abdallah na
mhasibu wa AMCOS hiyo, Bw. Kulwa Shinzi pamoja na wajumbe saba wa bodi ya chama
hicho.
Akizungumzia
kuhusu Ushirika, Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kufufua ushirika kwa
sababu ndiyo mkombozi wa wakulima. "Tumeamua kurudisha ushirika aminifu
kwa wakulima, na nirudie kutoa onyo kwa viongozi waliopata dhamana ya kuongoza
ushirika wasidhani kule wameenda kupata ulaji.”
“Tunataka
ushirika unaosimamiwa na viongozi waaminifu. Kwenye ushirika kuna fedha na kuna
mali za chama, kwa hiyo ni lazima tupate viongozi ambao ni waaminifu,” alisema.
Waziri
wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba alisema kuna tatizo katika uteuzi (grading) wa
tumbaku kwani wakulima wanalima tumbaku nzuri lakini katika upangaji bei,
wanalipwa bei ndogo. “Kuna wakulima wanakidai chama cha Mkombozi kiasi cha dola
za Marekani ambayo ni madai ya tumbaku waliyoiuza tangu mwaka 2014.”
Akizungumzia kuhusu Ushika Afya,
Dkt Tizeba aliongeza kuwa Tume ya maendeleo ya Ushirika kwa kushirikiana na
Mfuko wa Taifa wameunda mpango wa matibabu kwa wanachama wa vyama vya Ushirika
nchini ikiwa ni mafanikio yanayoendelea kuonekana katika kuimarisha Ushirika
nchini kwa kuakisi utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo ndiyo
mkataba kati ya wananchi na serikali katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020.
Alisema
kupitia utaratibu huo wanachama Wa Ushirika Afya atanufaika na huduma za afya
zinazotolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya zaidi ya elfu sita na
miatano (6500) vilivyosajiliwa na Mfuko Wa Taifa Wa Bima ya Afya nchini na
hatimaye kuchangia kikamilifu katika uzalishaji na ukuaji wa uchumi wa nchi.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment